Happiness Magese ni mwanamke pekee hapa Tanzania ambae amejitolea kuelezea ugonjwa huu wa endometriosis, kwa sababu umemsumbua tangu akiwa na miaka 13 kama alivyosema mwenyewe.Hapa Afrika na hata nchi zingine, wanawake wengi wanasumbuliwa na huu ugongwa lakini wamefanya siri.
Lakini tunaona jisi Hapiness magese alivyohamasisha wanawake kuupiga vita ugonjwa huu , alianzisha Hapiness magese foundation, kwa sababu ya ugonjwa huu wa endometriosis, sio kwa sababu aliwahi kuwa miss Tanzania na ni mlimbwende , bali na yeye ni mmoja ya wale wanaopata mateso ya ugonjwa huu.
Labda unaweza kujiuliza hili neno ni nini nsa ni ugonjwa gani.
Endometriosis ni ugonjwa ambao huhusisha seli zinazofaa kukaa ndani ya mji wa uzazi , badala yake seli hizo zinakaa nje ya mji wa uzazi. na unaonekana tu pale mwanamke anapoingia kwenye hedhi kila mwezi. na huanza tu pale mwanzo kabisa mwanamke anapovunja ungo.
DALILI ZAKE
-Maumivu makali wakati wa hedhi.na hedhi kutokufuata utaratibu wake.
-Uchungu wakati na baada ya kufanya mapenzi.
-Maumivu wakati wa kwenda haja.
-Uchovu.
-Ni kama kisu kinakata, maumivu haya huwa hayaelezeki kwa kweli.
Kutokana na maumivu haya makali sana, kwa sababu tatizo hili ni la wanawake wengi, wataalamu mbalimbali wanashauri kubadilisha mtindo wa kula chakula, endapo wewe una matatizo haya. hapa chini naleta aina mbalimbali za vyakula ambavyo vitakusaidia kuondoa maumivu makali.
1.Kula samaki wa baharini.
Samaki hawa ambao nitakuonyesha hapa wana vitamini nyingi , vitamini D ya juu .na samaki wengine wenye mafuta kama sangara , samaki wa maji baridi ni mzuri.
samaki huyu akikatwa ndani ni mwekundu, kuna mwingine sio mwekundu , lakini anafanana na huyu samaki.
Samakini mwingine ni yule mwenye mafuta .
2.Kla pilipili hoho:
pilipili hoho zina vitamini kwa wingi, vitamini C. na hii vitamini ndio hasa inahitajika kwa wale wote wenye tatizo la Endometriosis. na wale wenye uvimbe. mchanganyiko wake ni mzuri na hasa kama utatengeneza saladi .
3.Zabibu.
Zabibu za aina zote hasa zile nyeusi , kula mara nyingi uwezavyo ,kama huwezi kupata kirahisi , basi angalau ule hata mara 3 kwa wiki, zinasaidia kuondoa maumivu na kuponya magonjwa mengine ndani ya mji wa uzazi.
4. Kula mbegu za maboga, ni chakula kizuri na ni kinahitajika kwa ajili ya kusaidia endometriosis. na pia kina kiwango cha juu cha Omega3. na kina fatty acid ambavyo ni msaada mkubwa kwa ugonjwa huu.
5.Spinachi.
Kumbuka spinachi ni chakula kizuri pia na kinasaidia kuweka homoni zako vizuri. zina madini ya chuma mengi , ni mboga inayopatikana kirahisi tu.
unaweza kutengeneza saladi ya mchanganyiko wa vitu vyote .
– unaweza pia kusoma,
shirikisha marafiki na wale ambao unawafashamu wanasumbuliwa na matumbo ya hedhi.toa maoni yako.
No comments:
Post a Comment