Nafikiri hakuna mtu ambaye anapenda kuambiwa kuwa hana akili. Mara nyingi watu wanawaambie wengine kuwa hawana akili. Hakuna mtu asiye kuwa na akili . kila mtu ana akili.
Wengi hufikiri kuwa kusema hivyo itarekebisha tabia kuliko kuwaadhibu kwa njia nyingine, wazazi wengi huwaita watoto wao mbwa, paka, mbuzi.
Wengine hutumia neno la huna akili kwa kuelezea kuwa hawakubaliani ni kitendo kilichofanyika
Aibu inatokana na wewe mwenyewe, kutokuwa na uhakika na tabia yako. Ni tofauti na Hatia, Kitu kinachokutesa wewe mwenyewe , kwa mtazamo wako mwenyewe na unawadhuru wengine.
Aibu inabadilisha au kufuta Tabia? Jibu linategemea na lengo . Kwa watu wanaojali kuhusu mitazamo ya wengine juu yao, Aibu inaweza kufuta tabia mbaya. Ni aina ya Adhabu, Aibu ni kitu ambacho watu wengi hukiepuka. Ingawa kuna faida ndani yake.
Woga wa kukataliwa unaleta mtu kujiona kutengwa na kukosa nguvu ya kujitawala katika kisaikolojia, kimwili na katika ustawi.
Ukiwa unamwambia mtoto kila siku hana akili na kumuita majina ya ajabu, hio sio aibu ya mtoto peke yake. ni Aibu yako. Kwa sababu ataweza akawa na tabia isiokubalika katika jamii.
Aibu inaweza kukuonyesha jinsi ulivyo kuliko jinsi unavyotenda mambo. Hakuna lengo lolote lililopo hapo. Kama hisia zingine zilivyo, Aibu inaweza kuishi muda mrefu ndani ya mtu.
Aibu ni kitu kibaya, sio kitu cha kukubalika. Kwa ufahamu wa wazi tabia hio haikubaliki kwa sababu mara nyingi inakufanya ujisikie kuwa mwenye Hatia. Kitu ambacho kinaweza kusababisha Huzuni au stress mbaya.
Ni vizuri kama utaanza kumtia mtu moyo kwa kujitamkia maneno mazuri na kujipongeza wenyewe wanapokuwa wamefanya kitu fulani kizuri. Aibu inaondoa heshima ya mtu. Inashusha hadhi ya mtu. Kwa hio jitahidi kuangalia ni aina gani ya aibu iliopo ndani yako . shughulikia mapema. inawezekana kuondoa. Habari njema ni kwamba kinyume cha aibu ni ujasiri.
No comments:
Post a Comment