PAZIA ni miongoni mwa mapambo yanayotumika katika kupendezesha na
kukoleza umaridadi wa ndani ya nyumba. Kama ilivyozoeleka, pazia
zimekuwa zikitumika kupamba mlangoni na madirishani pia hasa maeneo
ambayo chumba tunapoishi kinakosa faragha.
Lakini pia, katika sehemu zenye joto kali ambazo mara nyingi madirisha
yake huwa na wavu au matobo, pazia imekuwa ikitumika wakati mwingine.
Halikadhalika, hata katika sehemu ambazo madirisha yake ni yale yasiyo
na wavu, bado wanatumia pazia kama pambo la kupendezesha nyumba na miaka
ya hivi karibuni limekuwa likitumika zaidi kuliko ilivyokuwa hapo
zamani.
Na kwa sababu imezoeleka kwamba mwanamke ndiye anayesimamia mambo mengi
nyumbani, pale inapokuwa haijapambwa na pazia ikapambika, huonekana kama
hawajibiki ipasavyo katika majukumu yake kama mama na msimamizi wa
uzuri na ubora wa makazi yake.
Mbali na nyumbani, pia pazia hutumika kupamba ofisi, hotelini na sehemu
nyingine nyingi. Pazia za ofisini zinafahamika na zile za hotelini
kwenye sehemu za vinywaji nako ziko za kupapendezesha.
Kadri ukuaji wa sayansi na teknolojia unavyochukua nafasi yake,
kadhalika maisha nayo yanabadilika ama kuboreka zaidi huku huduma na
bidhaa zikiboreshwa kila wakati.
Siku hizi tofauti na miaka ya nyuma, baadhi ya familia hupendelea hata
wakati mwingine ndani ya nyumba kunapokuwa na pazia ng’aring’ari zenye
mvuto, hulazimika kugharimia kuweka kiyoyozi ili pazia zisivurugike
katika mpangilio na kuharibu muonekano mujarabu wa ndani wa nyumba kwa
kisa tu kutafuta hewa.
Kwa ujumla pazia katika kipindi hiki cha kasi ya ukuaji wa sayansi na
teknolojia, zinatengenezwa katika aina au mitindo yenye mvuto tofauti na
hivyo kutoa fursa kila mtu kuchagua aina inayomfaa hasa kwa kuzingatia
mandhari iliyopo ndani ya nyumba yake.
Zipo pazia zilizotengenezwa kwa kutumia kitambaa kizito zaidi, za
vitambaa vyepesi, hariri, zipo za turubai, shanga, fimbo za plastiki na
hata za nyuzi.
Lakini pia zipo pazia ambazo zina matundu lakini zote kwa ujumla wake
zimekuwa zikitumika kupamba nyumba, ofisi ama hoteli kulingana na
mahitaji ama mandhari iliyopo katika sehemu husika.
Lakini pamoja na hayo uchaguzi wa rangi na aina ya kitambaa kwa wale
wanaopendelea kushona, nalo ni jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa na
wakati wa kufanya hayo yote kuzingatia aina ya rangi zilizopo katika
nyumba unayoilenga kuanzia ukutani na vitu vingine vilivyomo ndani.
Kikubwa zaidi ambacho nimependa kuzungumzia pazia, ni kutokana na
umuhimu wake katika kupendezesha makazi, ndiyo maana kuna umuhimu zaidi
hasa kwa kina mama kuzingatia vigezo mbalimbali wanapofanya uchaguzi wa
pazia hizo.
Ni vema kutambua kuwa ubaya wa nyumba yako utatokana na namna
unavyoitengeneza na hata mvuto wake pia utatokana na namna unavyochagua
na kupangilia wewe mwenyewe.
Ni jambo la aibu kuona unasifia mvuto wa nyumba ya jirani eti tu ameweka pazia nzuri, wakati na wewe mwenyewe unaweza.
Naamini kila kitu kinawezekana ukijipanga usitumie gharama kubwa katika
kupata pazia bora unazozipenda kama utajipanga na kudhamiria kuwa
nazo.
Wapo wanawake na wanaume ambao wanaweza kutundika pazia zao ndani ya
nyumba kwa kutumia kamba za kawaida na ikapendeza lakini nashauri kama
inawezekana si vibaya kutumia fimbo ama vibanio vya kutundikia pazia
hizo vinavyouzwa madukani.
Fimbo hizi hupatikana kwa wingi katika maduka ambayo yanauza pazia kwa
hiyo ni vema wakati unanunua pambo hilo ukatafuta na fimbo yake.
Ulizia fimbo au bomba ambazo rangi zake zinaendana na rangi iliyopo
kwenye nyumba pamoja na iliyopo kwenye pazia. Mara nyingi bomba za
kahawia, rangi ya maziwa na nyeusi isiyokolea hupendezesha.
Kwa kupata matokeo epuka rangi zinazong'ara kupindukia kwa sababu hazina utulivu, ni vema kuchagua rangi iliyopoa.
Zingatia kuweka pazia katika fimbo au bomba laini ambazo hazikwaruzi ili
zisizisoharibu wakati unavuta kuziweka sawa ama unazitoa kuzifua ama
kuondoa vumbi.
Zungumza na wataalamu wa urembo na mapambo ya nyumba ili kukupa ushauri
zaidi. Suala la msingi ni kufahamu mbinu za uwekaji wa pazia. Kumbuka
kuchanganya kama ni jepesi weka lenye lesi ndani.
Wakati mwingine ni vyema kubebesha pazi zito na lile la lesi ili joto linapozidi ulifungue mojawapo kupata hewa safi na mwanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients
Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...
-
:Kumbe Ukosefu wa Makalio Makubwa Unawafanya Wanawake Wasijikubali Unahisi kwanini
-
huwa tunakuletea Mishono mbalimbali ya nguo,leo tuna mishono ya lace ,vitenge na satin.Naomba kuiita hii peplum new level wengine waita pep...
-
Mwanamke Kitenge,Ni Ukweli Usiojificha Kuwa Vazi La Kitenge Halitotoka Katika Fashion. Unaweza Kushona Gauni Fupi Kama Hili ...
No comments:
Post a Comment