Thursday 2 August 2018

Huyu Ndio Mwanaume Amtakaye Mrembo Sanchoka


MWANAMITINDO mwenye umbo matata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ametaja vigezo vya mwanaume ambaye angependa kuwa mume wake.

Akizungumza na gazeti hili, Sanchi alisema kuwa anapenda sana mwanaume mwenye muonekano wa kimazoezi na pia mwenye kujielewa na kuweza kutafuta kwa hali na mali ili maisha yaeleweke.

Akizidi kutiririka, Sanchi alisema kuwa hapendi mwanaume ambaye amevutiwa kwa kumuona kwa umbo na sura yake bali mwenye kumpenda kweli kutoka moyoni.

“Unajua mwanaume anaweza kukuona akakutamani tu lakini anaweza akawa hana vigezo kabisa, kwangu mimi mwanaume mwenye muonekano wa kiume na mtafutaji ndiyo mwenye nafasi kwangu lakini mimi siangalii sura,” alisema Sanchi huku akisema mwanaume huyo bado hajampata hadi sasa.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...