Wednesday, 1 August 2018

Njia za Asili za Kuondoa Rangi Kwenye Viwiko vya Mkono na Magotini

Unaweza kuwa na ngozi laini sana kwenye uso wako au mwilini kwako lakini kuna baadhi ya maeneo ni tofauti hasa viwiko vua mikono na magoti.

Kwingine kote kunaweza kuwa laini lakini sehemu hizi mbili unaweza kuzikuta na weusi, ngozi haiko sawa na hata kuwa na vipele au unakuta pamebabuka, ngozi kutokatoka, kimsingi ngozi ya kiwiko na goti huwa siyo laini.

kutokana na ugumu wa sehemu hizo, baadhi ya watu huona hata aibu kuvaa nguo zinazoonesha kiwiko au magoti, lakini kama na wewe ni muhanga, basi leo tunakupa vidokezo vya tiba ambavyo unavipata jikoni kwako ili kukusaidia kuifanya ngozi ya kiwiko na goti kuwa nzuri.

Angalizo; sehemu hizi zina ukosefu wa tezi za mafuta kitu kinachofanya ziwe kavu haraka na hadi kuwa nyeusi kuliko kawaida. Mara nyingi wengi wetu hizi sehemu huwa hatuzijali, tunaziacha zenyewe unakuta lile tabaka la ngzi linakufa na haliondolewi na kufanya pawe pagumu na pakavu.

Vile vile mkusanyiko wa seli zilizokufa kwenye sehemu hizi husababisha ngozi kutokuwa katika hali nzuri, na hilo tabaka la ngozi inatakiwa kuondoloewa mara kwa mara ili kuihuisha ngozi upya.

Cha kufanya basi ili kutoa huo ugumu na weusi wa magoti na viwiko vya mikono, unaeza kufanya vifuatavyo.

Skrabu ya Sukari; skrabu inasaidia kuondoa na kubandua seli zilizokufa ambazo zinasaidia seli mpya kutengenezwa na kufanya ngozi kuonekana nzuri na laini. Changanya kijiko kimoja cha asali na sukari ya kawaida, pakaa/sugulia kwenye goti lako au viwiko vya mikono kwa mwendo wa duara, sukari itasaidia kutoa ngozi ambayo haitakiwi, kisha osha na majisafi, unatakiwa kufanya hivi kwa wiki mara moja.

Limao na juisi ya viazi ulaya; viazi ulaya na limao vina viambata vya blichi, ambazo inazifanya ziwe chaguo la wengi kwenye mambo ya urembo. kata limao nusu sugulia kwenye kiwiko na magoti au kata pia kipande cha kiazi mviringo na ufanye hivyohivyo  na limao, hii itasaidia kufanya ngozi hii iwe nyepesi zaidi. Kisha tumia asali ambayo itasaidia kufanya ngozi kwa unyevunyevu.

Mafuta ya kukandia; mafuta yanaingia kwenye ngozi na kukusaidia kuifanya ngozi kuwa na unyevunyevu wa asili, sababu hizi sehemu hazina tezi za mafuta kwa kuzikanda na mafuta mara kwa mara na mafuta ya zeituni, lozi au nazi. Mafuta ya nazi husaidia pia kung’arisha, hivyo kanda na aina mojawapo ya mafuta na yaache yaingie kwenye ngozi. Tumia dodoki au jiwe lile laini; ukioga unaweza tumia jiwe lile laini; ukioga waweza tumia jiwe laini au dodoki kusugua sehemu za magoti na viwiko vya mikono, usisugue kwa nguvu, taratibu itasaidia kubandua ngozi iliyokufa, siyo lazima kufanya kila siku unaweza  pata vidonda na ukiwa unasugua fanya kwa mwendo wa mduara.

Kuifanya ngozi nyevunyevu; chukua mafuta yako paka kwenye ngozi ili kusaidia peaendelee kuwa laini, baada ya hizo tiba zote, ukishafanya hivyo hakikisha huachi magoti yako na viwiko bila kupaka mafuta hii itasaidia pasiwe pakavu na mbaya au kakamavu.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...