Wednesday, 1 August 2018
VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUISHI BILA MARADHI.
Kundi moja la wataalamu wa moyo limeelezea masuala muhimu ambayo yanamsaidia mtu kuishi maisha marefu kama ifuatayo:-
1. Jiweke mbali na sigara.
2. Epuka unene.
3. Fanya mazoezi.
4. Kula lishe bora.
5. Hakikisha unacheki na kupima kiwango cha kolestero mwilini, shinikizo la damu na sukari na kuhakikisha viko katika kiwango kinachotakiwa.
Uchunguzi huo umeonyesha kwamba watu wengi umri wa kuanzia miaka 50 ambao wanaishi kwa kufuata masharti hayo huwa na uwezo wa kuishi miaka 40 zaidi bila kupata shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo, ambayo ni magonjwa makuu mawili yanayoua watu zaidi duniani. Wataalamu wamesema kwamba, kila mtu anayetaka kuishia maisha marefu anatakiwa kufuata ushauri ufuatao:
• Jiepushe kuvuta sigara au acha kuvuta sigara kabisa.
• Hakikisha BMI yako haizidi 25.
• Kila wiki pata dakika zisizopungua 150 za kufanya mazoezi ya kawaida.
• Jitahidi kufuata maelekezo ya kula lishe bora ambayo ni:
vikombe 4 na nusu vya matunda na mboga mboga kwa siku, samaki mara mbili au tatu kwa wiki. Usinywe sana vinywaji vyenye sukari, kula vyakula vyenye ufumwele kila siku na chumvi isizidi miligram 1,500 kwa siku.
• Kiwango cha kolestero au mafuta katika damu yako kisizidi 200.
• Shinikizo lako la damu lisiwe zaidi ya 120 chini ya 80.
• Sukari katika damu iwe chini ya 100.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients
Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...
-
:Kumbe Ukosefu wa Makalio Makubwa Unawafanya Wanawake Wasijikubali Unahisi kwanini
-
huwa tunakuletea Mishono mbalimbali ya nguo,leo tuna mishono ya lace ,vitenge na satin.Naomba kuiita hii peplum new level wengine waita pep...
-
Mwanamke Kitenge,Ni Ukweli Usiojificha Kuwa Vazi La Kitenge Halitotoka Katika Fashion. Unaweza Kushona Gauni Fupi Kama Hili ...
No comments:
Post a Comment