Monday 6 August 2018

DONDOO ZA UREMBO NA UTANASHATI NDIO PAKE HAPAAAA!YESSSS. LEO NATAKA NIKUJUZE NAMNA YA KUFANYA NGOZI YAKO KUWA SOFT,NZURI,TAMU KAMA YA MTOTO MCHANGA ALIYEZALIWA LEO NA KUKUFANYA KIVUTIO KWA WATU PINDI WANAPOKUONA.


NISIKILIZE MIMI NIPO KWA AJILI YAKO BEST YANGU WA UKWELI
Sasa leo nataka nikujuze kuhusu Scrub ya nazi(Coconut Scrub).
Hivi unajua kuwa unaweza kuwa mrembo kwa kutumia vitu vya asili tu?. Ndio inawezekana!. Wengi wetu tumekariri kwamba, ili uwe mrembo na mwenye muonekano wa kuvutia machoni pa watu,basi ni lazima utumie vipodozi vya madukani, vyenye kemikali za sumu. Na vipodozi hivi vinauzwa kwa bei ghali kweli. Na wakati mwingine usipate hata matokeo uliyokuwa unategemea. Unakuwa umepoteza pesa na umezidi kuharibu muonekano wako wa asili.
SASA LEO NITAWAELEZA maajabu ya nazi katika urembo. Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza ikatumika kama scrub ya ngozi yako.
Fuata hatua hizi hapa chini ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini,nyororo na wenye mvuto.
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini kwa leo nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.
NINI CHA KUFANYA:
1. Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri na ili upate matokeo mazuri jitahifi kuikuna taratibu ili itoke laini.
2. Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
3. Kausha uso wako kwa taulo safi.
4. Baada ya uso wako kuwa mkavu, ichukue ile nazi yako uliyoikuna tayari, taratibu anza kusungua usonio kwa dakika kama 3 mpaka 5.
5. Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
6. Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida.
7. Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote.
Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yani mara moja kwa siku. Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako.
NI HAYO TU KWA LEO

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...