Thursday, 7 June 2018

Njia 10 Za Kukufanya Uwe Mtu Bora

Kujijali.  Kujijali ni sehemu moja kubwa sana kwenye maisha ya mwanadamu , hasa kwa yule ambaye yuko bize na kazi nyingi za kila siku.
selfcare_selflove-870x330 Njia 10 Za Kukufanya Uwe Mtu Bora
Kujijali ni kitu gani? ni hali ambayo inahitaji kupata muda wa kutulia ukiwa mwenyewe kwa ajili yako na maendeleo ya maisha yako badala ya kusubiri mtu mwingine kukujali wewe.
Mara nyingi watu wanauliza unawezaje kujijali  ukiwa na majukumu ya kuhudumia wengine ? Jibu ni kwamba , huo ni mtazamo wa mtu . Lakini kama utafahamu kutumia muda wako vizuri unaweza kuchukua nafasi kwa ajili yako. Unatafuta muda katikati ya muda wako kutulia kila siku kwa dakika kadhaa  mahali ambapo  pana utulivu   ili kuongeza nguvu mpya, mawazo mapya . Utatumia muda wako kwa kukaa tu bila ya kufanya kitu , ukiwa umetulia .
Ukiwa unafanya hivyo kila siku , hautakuwa na stress za aina yoyote , bali utaishi maisha bora.
Hapa chini kuna njia 10 za kufanyia mazoezi ya kukufanya ujijali.
1.Kujijali maana yake ni kujitambua wewe ni nani na una mipaka gani
Ni kutambua wakati unapokuwa umezidisha kitu katika majukumu yako . umepitiliza kiwango cha kile unachotakiwa kufanya.  Ni kuelewa namna ya kurekebisha yote ambayo yanakutatiza.
2.Kujijali maana yake ni jinsi unavyojiona mwenyewe.
Kujua matumizi ya muda, kufafamu muda wako wa kupumzika  na wa kulala na muda wako wa kufanya kazi , Kufahamu ratiba yako ya kila siku, ya wiki, ya mwaka. Na kufahamu jinsi ya kutunza mwili wako , Akili yako na Roho yako. kujipenda, kujithamini, kujiona mshindi kuanzia ndani mwako.
3.Kujijali ni Kumpenda Mungu, Kuwapenda watu na kuipenda nafsi yako.
Chochote unachopenda ufanyiwe wewe, jaribu kuwafanyia wengine. Ukimpenda Mungu kwa nguvu zako zote, akili yako yote, moyo wako wote na roho yako yote, na kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Kuacha kula vitu ambavyo sio salama kwa afya yako. kuacha dhambi ili kuondokana na hofu , mashaka mbalimbali kwenye maisha yako.
4.Kujijali maana yake ni Kuishi Wakati Uliopo
Watu ambao wanasubiri kufanya kitu baadae , hawajijali na wala hawajitambui. Una masaa 24 kila siku kwa nini  usitumie muda wako kufikiri mambo yaliopo wakati huo. Utakuta mtu ana kitu cha kufanya lakini anasema nitafanya kesho, wakati uwezo wa kufanya hicho kitu anao. Unapoteza muda mwingi sana . Utashindwa kujijali mwenyewe. Kama huna Nidhamu ya mitandao huwezi kuishi wakati uliopo. kama hutumikishi mwili wako sawasawa hutaweza kuishi wakati uliopo. Watu wengi wanaugua magonjwa ya kutofanya kazi za kutosha.
Kama huna kazi za kutosha nitafute nikufahamishe kazi za siku nzima, ambazo zitakufanya ujione nawe unaishi.
5.Kujijali maana yake ni kutoa wazo ambalo litatatua Hali ngumu ya kazi uliyonayo.
Tunafahamu ni kitu gani tunahitaji na nini cha kushughulikia. Kipo kitu ambacho kinaweza kufanya kazi yako  iwe rahisi, njia hio ni kufanya kitu unachokipenda. Mahali ambapo utajisikia vizuri kila unapokuwepo kazini kwako, masaa unayotumia kazini kwako, muda wa kujisomea , muda wa kula na muda ambao sio wa kula. Unajitawala mwenyewe. Wewe ndiye mkurugenzi wa maisha yako, na ni Raisi wa muda wako.
6.Kujijali maana yake ni kupata muda wa kujifahamu vizuri.
Kujiwekea mipaka yako, kutambua wakati umezidiwa na kitu na kukirekebisha haraka , Kutambua hisia mbaya na nzuri zinazojitokeza kwako na kama ni mbaya unakabiliana nazo mara moja. Kumsikiliza Mungu zaidi kuliko kusikiliza watu.
7.Kujijali maana yake ni kujua kitu kinachokufurahisha na kitu ambacho kinakutoa kwenye hali ya amani.
Kuzitambua hisia ambazo sio zako na kuziondoa , kutengeneza tabia nzuri kila siku kwa kusoma Neno la Mungu zaidi na kujitahidi kuhudhuria semina mbalimbali. Jaribu kuwa na mtu wa karibu ambaye kila ukimpigia simu  unafurahi kuongea naye. usiende sehemu ambayo itakukosesha amani
8.Kujijali maana yake ni kutopitia mahali ambako hukupanga kupitia .
Unaweza ukawa unarudi nyumbani ukitokea kazini , ukakutana na mtu akaanza kukushawishi kwenda Bar. kama hukupanga usiende.  huenda akakuambia mwende sinema lakini hukupanga, usiende.
9.Kujijali Maana Yake ni Kulisha nafsi yako kitu kizuri.
Hii ni pamoja na kufanya tafakari, kuomba, kutembea   kwa muda wa dakika 30, kuhudhuria ibada, semina. kuwa mtu wa shukurani, kusoma na kusikiliza kitu ,
10.Mwisho , Kujijali ni Kukuwa na muda wa kujipenda
Kutambua kuwa hakuna mtu  mwingine ila wewe, na wewe ni mtu sahihi . hakuna aliye sahihi zaidi yako. Wewe ni Bingwa wa Upendo.
Subscribe kupata makala mpya kila mara

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...