Nikiwa na umri wa miaka 20, pombe ilikuwa sio muhimu sana katika maisha yangu. Ilikuwa nikienda kwenye sherehe, lakini sikuweza kutumia pombe.
Lakini kadri siku zilivyoendelea , niliamua kujaribu. Nikawa muathirika mkubwa wa pombe, nilifikiri ndio kitu kinachonipa furaha na utulivu. na kuamini kuwa pombe ndio suluhisho la matatizo.
Lakini nilikuja kujitambua nilipofika umri wa miaka 37, Sikutumia tena. Inashangaza, nikawa huru kabisa bila ya pombe. nikawa na furaha na nikawa mzuri . Ingawa sitaki kujilaumu, lakini natamani kama ningefahamu mapema kuwa Pombe sio nzuri na kupata uathirika wa kawaida . kama ningerudi kule nyuma , ningeweza kujiambia mambo haya kuhusu pombe.
1.Huhitaji pombe ili kupata furaha
Utaweza kucheka kwa furaha bila ya kutumia kilevi. Acha kutumia pombe kwa kutafuta furaha. Unaweza kuwa unaamini kuwa pombe ndio chanzo cha furaha yako. Hio sio kweli. pombe haifanyi kazi yeyote ya kuleta furaha au kufanya mambo kuwa bora. Itakuletea hisia tofauti katika akili yako na kufanya mambo yasio na tija. Kumbukumbu zako nzuri zinazotokana na mahusiano yako, ucheshi wako, mawasiliano mazuri, yote hayo yanawezekana bila ya pombe.
2.Kuwa na Ufahamu wa Mahusiano yako bila ya pombe.
Katika jamii yetu, unaweza kuona kuwa ni rahisi kujiingiza kwenye maisha ya kunywa kila siku. Lakini tabia hio itakusababishia matatizo baadae. kuwa makini na unachokitumia kwenye mwili wako, katika kila hazina yako, hasa katika kuzoea kitu. kumbuka kuwa uharibifu unatokana na unywaji wa pombe au kutumia kitu isipokuwa kawaida.uwe makini na ujijali mwenyewe.
Unaweza usitambue kitu sasa kwa kuwa bado ni mdogo, na una miaka 20, lakini hata kutumia pombe kidogo kidogo kila mara , utaingiza kitu cha kutosha . utakuwa hupati usingizi wa kutosha, kuwa na uzito zaidi, kuzeeka haraka, kupata kiarusi,kisukari na mwisho ni kufa muda usio wa kwako.
3.Sex ni bora bila ya pombe
Watu wengi hufikiria kuwa ukitumia pombe utafurahia ngono. Itakupunguza kabisa, itashusha nguvu zako chumbani. ukweli ni kwamba pombe inaharibu hisia zako za kweli, hisia za mguso, utendaji wako utapungua kila siku.
Pombe kwa mwanaume ni tatizo kubwa, kwa sababu inasababisha kushindwa kusimamisha uume kwa kawaida. wanawake na wanaume wote hupenda kupata mapenzi yenye kutosheleza, Na hio utapata bila ya pombe.
Ubongo wako utaanza kushindwa kufanya kazi, utakosa uwezo wa kupokea taarifa kutoka kwenye hisia zako. ubongo utaanza kupokea taarifa kwa taratibu sana kutoka mwilini mwako. Utashindwa kuelewa ni kitu gani kinatokea. kumbuka kuwa ni kutokana na pombe.
Lakini ukiacha , mwili wako utashirikiana vizuri na ubongo na kujikuta unafurahia maisha yako ya sex kila siku . Mawazo yako yatakuwa ya kushangaza kila wakati.
4.Pombe Haiondoi na wala kupunguza Misongo ya maisha
Ni mawazo mabaya kufikiria kuwa pombe inasaidia kupunguza mawazo. Lakini kama unajiona hivyo , ni kwa muda mfupi sana. uwazi huo unabaki palepale. woga wako, wasiwasi wako utabaki pale .Huko ni kujipa tumaini na kuamini kitu ambacho sio sahihi.
Ukweli ni kwamba unapokuwa umelewa,Labda uwe umefanya kitu fulani cha maendeleo yako,Stress zako zitabaki hapo. Unachokifanya kwa kunywa ni kujenga uvumilivu na kutengeneza tatizo jipya kwa ajili yako.
Njia pekee ya kupunguza stress ni kushughulikia chanzo cha tatizo. kuliko kuepuka tatizo kwa kunywa pombe. labda umeachana, umefukuzwa kazi, uko kwenye mahusiano mabaya, pambana na hali hizo , Halafu uweze kuondoa yaliopita na kupata ukweli wa utulivu bila ya kutumia pombe.
5.Kutumia pombe kwa ajili ya kupunguza maumivu ni hatari zaidi
Pombe ni njia ya uongo. Itakushauri kuwa ni muda wa kusahau maumivu. kunywa zaidi na utasahau kila kitu. utaharibu mfumo wako wa Nevo, Utaongeza hisia za woga, wasiwasi, kitu ambacho utaona vigumu kuondokana na stress za kila siku. kama kilikuwa kidogo kitazidi kuwa kama mlima.
Utaanza kuzidiwa na majaribu, hata kama ni madogo. Kwa sababu pombe itakufanya ufikirie kuwa bila hio hutaweza kufanya kazi kwa siku nzima. Utakuwa unapata usingizi kidogo tena wa ghafla tu, mara ukiamka unajiona uko vile vile. Pombe inakuibia furaha yako ya kweli, upendo wako wa kweli. Maisha yako ya kweli.
Maisha ni mazuri bila ya pombe.Naamka kila siku nikiwa na akili nzuri, Nafahamu nilichokifanya kabla. ni mkweli. nina hisia za kweli na za kutosha kila siku na kufurahia kila dakika inayokuja kwa ukamilifu na utoshelevu.
No comments:
Post a Comment