Thursday 7 June 2018

MAGONJWA YA SARATANI: Mambo Ambayo Unaweza Kuyafanya Kila Siku Ili Kuzuia Saratani

1-1-2 Mambo Ambayo Unaweza Kuyafanya Kila Siku Ili Kuzuia Saratani
Pamoja na kwamba unakubaliana na dawa nyingi zinazookoa  maisha , matibau ya saratani, Nataka tuende ndani zaidi. huko ambako dawa zinafanya kazi . Ni kuangalia kiini cha tatizo, kuangalia zaidi subira badala ya kuangalia ugonjwa.
Pamoja na kutumia dawa inahitajika kuwa na uchunguzi zaidi katika safari hio ili kujifunza  baadhi ya mambo ya kuponya.
Kwa mfano kuwa na subira,  kabla hujaanza kupata dawa, ni vizuri kwenda kucheki , hii ni sawa lakini  kucheki wakati mwingine haizuii ugonjwa.  Watu wengi wamekuwa katika hali ya kutaka kujua , na inasaidia  sana kama ukiwahi kugundua tatizo. Lakini  hali hio haizuii   saratani  inapoanza .
Kwa Hio Tunaepukaje Saratani?
Ni katika kubadilisha mtindo wa maisha. Ukichagua mtindo mzuri wa maisha utajilinda na ugonjwa wa saratani. Kujifunza kuwa na subira . Kumbuka ugonjwa hauji siku moja , ni kutokana na maisha yako uliyonayo. Ukibadilika utaboresha maisha yako ya kila siku.
Utafanyaje Kila Siku Kujilinda Na Saratani.
Kujilinda na saratani ,Kitu cha muhimu sana ni kujifunza hali yako ya mwili na mazoea uliyonayo. Sababu mbalimbali zinazosababisha, Mazingira, na maumbile.Kwa kuona hivyo,  Utaweza kubadilisha mtindo wako wa maisha ambao utapunguza  hatari ya  kupata ugonjwa.
Zipo njia rahisi na zenye nguvu ya  kutengeneza afya . Ni katika kuondoa yasiofaa na kuweka yanayofaa. Kwa mtazamo huo usirudishwe nyuma na kitu chochote kile anza kufuatilia  mtindo mzuri wa maisha.
The-Top-10-Vegetables-High-In-Protein Mambo Ambayo Unaweza Kuyafanya Kila Siku Ili Kuzuia Saratani
Kula Mlo kamili
Chagua kitu halisi, kamili, chenye lishe nzuri, cha mimea na chagua nyama ilio bora kama kuku wa kienyeji. vyakula ambavyo bibi  na babu walikuwa wakivitumia. Achana na vyakaula vya kisasa, vya kwenye makopo.  tengeneza chakula chako kiwe na rangi nzuri ya mimea, protein ya kawaida, na mafuta mazuri,  vyakula vya kupaki vyenye sukari achana navyo.
Usaidie mwili wako  kwa kuondoa sumu nyingi mwilini  .
8-1 Mambo Ambayo Unaweza Kuyafanya Kila Siku Ili Kuzuia Saratani
Mbinu nzuri ni kula vyakula vingi vya mizizi na kufanya mazoezi  ili mwili utoke jasho. Ondoa sumu kwa kula mbogamboga  na matunda,  hasa wakati wa asubuhi unaweza kula kabichi ya kutosha, au broccoli kwa ajili ya lunch, na ukala wali kidogo jioni  na mboga za kutosha. tumia vyakula jamii ya kunde mara kwa mara.
Punguza sumu Kwenye mazingira yako.
Hewa chafu, madawa ya kuulia wadudu,  mercury inayopatikana kwenye vipodozi na sehemu zingine . hivi vinasababisha sana saratani ya kibofu cha mkojo na saratani ya matiti , mirija ya uzazi.  huwezi kuepuka vyote lakini unaweza kupunguza baadhi ya chemicals kwa kufanya uchunguzi wako mwenyewe.
Jali mwili wako, hasa utumbo wako.
Ndani ya tumbo lako kunahitaji afya ya hali ya juu.  unaweza kutafuta mbinu za kusafisha  sumu ilipo ndani yako. Tumia Dawa za antibiotics panapokuwa na umuhimu huo tu.  Tena tumia zenye sifa na kuongeza  kula chakula unapokuwa unatumia ili kusaidia  kazi ya dawa hizo.
Vyakula vizuri vya kutumia mara kwa mara ni kama viazi vitamu, karanga,  na mbegu za maboga.  Mizizi inasaidia kuweka tumbo lako vizuri.  utumbo unakuwa na afya nzuri .
Achana na Stress
Mtu mwenye stress anakuwa yupo kwenye hatari ya magonjwa mengi. Kumbuka kuwa stress inatokana na mambo mengi. Mahusiano mabaya, maisha sio mazuri,  mawazo mabaya, kazi ambayo huipendi,  yote haya yanaweza kusababisha saratani  au ugonjwa wa akili.  lakini ipo mbinu ya kuondoa au kupunguza . Nayo ni Meditation na mazoezi. tafuta mbinu ambazo zinafanya kazi kwa ajili yako na ufanye mara kwa mara.
Mazoezi ya kutembea kwa muda wa dakika 45 ni mazuri.  fanya mazoezi kila siku au kila baada ya siku  moja ili kujiepusha na saratani. wakati huo huo zingatia kutumia vyakula kama dawa.  kwa kufanya hivyo utajiboresha katika kila vipengele vya afya ya mwili wako.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...