Najua sukari ina utata, Kuna maswali mengi kuhusu vitu vitamu. Hapa kuna baadhi ya maswali ambayo yanakuumiza kichwa .
Sukari ya kwenye matunda ni sawa? Nimesikia sehemu kuwa ni nzuri, lakini nikasikia sehemu nyingine tena kuwa nikae mbali nayo , Nimepatwa na utata mkubwa. Na sasa sitaki kula ndizi.
Kuna Baadhi ya matunda yenye sukari kwenye mlo wa afya, lakini sukari ya matunda bado ni sukari. Sukari ikizidi huhifadhiwa kama mafuta. Nashauri kama una uzito mkubwa tumia matunda ambayo hayana sukari nyingi tena tumia kidogo.
Matunda ambayo hayana sukari nyingi ni kama Strawbberrie, raspberries, na blackberries , pears na apples.
Ndizi ni tundfa lenye kiasi cha juu cha sukari lakini lina kiasi kikubwa cha fibers. kwa hio usijisikie vibaya kutumia mara moja moja.
Kula Kipande cha chocolate kwa siku inaharibu afya yangu? Nimekuwa nikiepuka sukari lakini nakula kipande cha chocolate kila siku. Ni kweli ni mbaya ?
Chocolate , hasa ile yenye rangi nyeusi ina lishe nzuri. Chocolate ni chanzo kizuri cha madini ya magnesium na chuma. Chocolate inapunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kupunguza stress, na kukuweka katika hali nzuri.
Lakini unaweza kujaribu kutotumia kila siku, Anza kupita siku bila ya matunda au chocolate au kitu chochote kitamu , Halafu sikiliza mwili wako unajisikiaje. Huenda sio lazima kutumia kila siku.
Sukari ipi ni bora kutumia ambayo ni ya Natural?
Hapa Kuna baadhi ya aina bora.
Coconut Sugar. Sukari ya nazi ina madini ya antioxidants ambayo huwezi kuyapata kwenye sukari nyeupe.
Raw honey. Asali ghafi, ni asali ambayo haijachanganywa na vitu vingine. pata kutoka shamba moja kwa moja. Asali za kawaida. Lakini asali hii hairuhusiwi kutumia watoto wadogo, wanawake wenye mimba au wale vegans.
Lakini pia sio lazima kutumia kila siku. Ingawa sukari ya nazi ina fructose ya kiasi cha chini , asali ina asilimia 4o . Sukari ya mezani ina asilimia 50 ya fructose. Kwa hio kuwa makini katika kila matumizi ya sukari.
Nimepata Utata kuhusu Yogurt. Wengine wanasema ni nzuri , lakini wengine wanasema sio nzuri. Lakini zote zinaonekana kuwa na sukari ya juu. Watu wanasema tule yogurt kwa sababu ina afya. Nikienda kunua vitu natumia muda mwingi kusoma lables, mara nyingi natoka bila ya kununua chochote.
Ni vizuri kuchukua muda wa kusoma lables. napendekeza kutumia low-or full-fat yogurt kwa sababu hazina sukari nyingi. Yogurt ni chanzo kizuri cha protein ingawa hatuhitaji protein nyingi kupitia hizi yogurt. Hakikisha yogurt hio inatokana na ng’ombe wa kienyeji sio wengine, au inayotokana na matunda yasio na sukari nyingi.
Nitajuaje kuwa Aina hii ya sukari ni nzuri kwangu? Kwa sababu tunasikia sana kuhusu kutumia matunda mengi ni vibaya– Tunatakiwa kutumia hadi kiasi gani ?
Tunaweza kuwa na ufahamu na hata kula vyakula vizuri , Lakini kama tunasikia ndani yetu wasiwasi, kujilaumu, au kutumia muda mwingi kuhangaikia lishe nzuri katika vyakula vyetu, Hapo kuna umuhimu wa kufanyia kazi . Chakula cha shida bado ni shida, na sio nzuri kwa ajili ya afya yako au uzito wako.
Tutazame ulaji wetu kwa ujumla ukoje. tutazame nafsi zetu ,wasiwasi wetu , kujilaumu kwetu. Tunajisikiaje tunapokula. Kama moyo wako unasita kula kitu fulani usile. Na kama una uwezo jaribu kusikiliza mwili wako unahitaji nini.
Ni ushari wangu kama utaamua mara moja kwa wiki kutumia kitu kitamu , kuliko kutotumia kabisa . lakini tumia kiasi. na iwe ni utaratibu wako. Halafu rudi kwenye utaratibu wa tabia yako ya kutotumia vitamu.
Unaweza ukaona kama haiwezekani, lakini tunza list ya ushindi wako. Kila siku. Chagua kilicho bora.
Share kwa wingi.
No comments:
Post a Comment