KUNA mastaa ambao walijikuta wakiwaacha wengi midomo wazi kutokana na
kuwa na miili iliyoshiba lakini ghafla wakaonekana katika muonekano
tofauti wakiwa ‘wamepukutika’ na kuzua viulizo, huku wengi wao wakitoa
visingizio mbalimbali.
GIGY MONEY
Mwanadada huyu anayejulikana kwa jina halisi la Gift Stanford alitikisa
mno kwa muonekano wake, jinsi alivyokuwa amenona na kujazia kwenye
msambwanda, lakini kitu kilichowaacha wengi hoi ni baada ya kupukutika
ghafla, huku sababu mbalimbali zikitajwa,
ikiwemo kuharibika kwa mimba kadhaa na `stress’ za mapenzi na hadi sasa mwili wake haujarudi.
AUNTY LULU
Ni moja ya wadada ambao walikuwa gumzo kila kona, huku mara kadhaa
akijitapa kuwa wowowo lake ndo kila kitu maishani mwake, lakini siku
chache zilizopita mwanadada huyo aliibua
taharuki baada ya kuonekana akiwa modo na kalio limeiisha, huku akidai
ni kutokana na kufanya mazoezi, hivyo mpaka sasa hajarudi kwenye ubora
wake.
AMANDA
Msanii huyo alikuwa balaa kwenye suala zima la mvuto, mwili na shepu
yake alikuwa amefungasha vilivyo, lakini jambo lililoibua taharuki ni
baada ya kupungua huku watu wakimzushia mambo mbalimbali ikiwemo maradhi
ya kisasa, jambo alilolipinga
vikali, ila hadi wakati huu ameshindwa kurejea kama zamani.
BABY MADAHA
Bishosti huyu ambaye naye alikuwa kibonge mwepesi lakini ghafla
akapukutika, huku mwenyewe akidai ameamua kuwa modo sababu anaupenda
mwili huo kuliko akiwa bonge na hadi sasa amebaki katika hali hiyo ya
umodo. RAY C Anaitwa Rehema Chalamila ni moja ya wasanii wenye sauti
mwanana ya kumtoa nyoka pangoni, bibie huyo kipindi kifupi cha nyuma
alikuwa kibonge na kuonyesha kutopendezwa na muonekano huo akawa
anajitahidi kufanya mazoezi mara kwa mara ili apungue na akafanikiwa,
hadi sasa amebaki kwenye hali hiyo ya wembamba.
AMBER LULU
Jina lake halisi ni Lulu Euggen `Amber Lulu’ kwa wanaomfahamu vyema
mwanadada huyu machachari, watakubaliana na mimi kwamba siyo Amber yule,
alikuwa ana mwili
wa haja na kajazia kinoma kwenye msambwanda, saizi imebaki stori tu.
Na MAYASA MARIWATA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients
Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...
-
:Kumbe Ukosefu wa Makalio Makubwa Unawafanya Wanawake Wasijikubali Unahisi kwanini
-
huwa tunakuletea Mishono mbalimbali ya nguo,leo tuna mishono ya lace ,vitenge na satin.Naomba kuiita hii peplum new level wengine waita pep...
-
Mwanamke Kitenge,Ni Ukweli Usiojificha Kuwa Vazi La Kitenge Halitotoka Katika Fashion. Unaweza Kushona Gauni Fupi Kama Hili ...
No comments:
Post a Comment