Leo
naonyesha mapishi ambayo mara nyingi tunakula tuendapo katika
restaurant kama Subway; Sasa hapa naonyesha namna ambayo unaweka pata
taste tamu zaidi hata ya kule restaurant. Pishi hili lahusisha mkate (
French bread) na beef.
Mkate ni wa kununua ila ipo siku nitawaonyesha namna ya wewe mwenyewe kuweza kuupika.
MAHITAJI
- Nyama steak nusu kilo
- Vitunguu maji viwili
- Pilipili Manga
- Mixed Hearbs
- Pilipili ya unga
- Cheese kwa wale wanaotumia
- Chumvi
- Unga wa ngano vijiko viwili
- Butter kijiko kimoja
JINSI YA KUANDAA
Hatua
ya kwanza kabisa ni kuchemsha nyama. Nyama usiikate kate chemsha ikiwa
nzima nzima – weka maji, weka mixed hearbs kijiko cha chai kimoja, weka
pilipili manga kijiko kimoja cha chai, weka pilipili ya unga nusu kijiko
cha chai. Sasa iache nyama hii ichemke kwa muda wa kutosha kabisa hadi
itakapokuwa imelaininka kabisa.
Nyama ikiwa tayari icharange kwa style ya slices – ikate kwa ulalo hivi yaani mapande makubwa ila membamba.
Sasa
chukua chombo zaidi iwe flampeni weka kwa moja kisha weka kijiko kimoja
cha butter na unga wa ngano ikaange hadi ngano iwe kama inakuwa na
brown hivi – kama ukiona inashika sana chini unaweza ongeza ile supu
uliochemshia nyama.
Kisha
weka vitunguu na pilipili hoho , kisha weka ile nyama – vikiwa
vinachemka ongeza pilipili manga na pilipili ya unga kidogo pia chumvi
kama ile ya supu haitoshi.
Kumbuka hii souse sio iwe maji maji so ikuwa ni nzito tu kama ambavyo
Ikiwa tayari chukua mkate wako upasue katikati weka nyama , pamoja na
vitunguu maji, vibicho au roasted , weka cheese , na majani ya
giligilani kwa aroma zaidi.
Tayari endelea kuenjoy mkate wako na beef.
No comments:
Post a Comment