Kuna
wakati katika leo tena tulikuwa tukipeana ideas namna ya kupangilia
kifungua kinywa.Lengo lilikuwa kubadilishana mawazo ili kuondokana na
mazoea ya kula kifungua kinywa hicho hicho kila siku.Tunaambiwa mlo wa
subuhi ndio unatakiwa kuwa mlo mkubwa kuliko mwingine lakini nyumbani ni
tofauti.Chai na mkate wa kwa mangi jioni sahani hiyoo ya ubwabwa na
maharage.Kina mama walikuwa wakituma mpangilio wa vitafunywa au namna
unavyoweza kuandaa kifungua kinywa kutokana na vyakula vinavyopatikana
katika mazingira yetu ya kila siku.
Tuna viazi vitamu hapa
Viazi vitamu sokoni viko tele,mihogo na hata magimbi.
Nikavimenya,nikaviosha na kuvikata hivi kwa sababu mie nilikuwa navikaanga,unaweza pia kuchemsha.
Tayari kuliwa na unaweza kula na kachumbari pia lakini mie sikuweka kachumbari.Sikuishia hapo…
Nikapika
chapati za maji,huu ni mkorogo wa unga wa ngano na maji baridi
niliweka,mayai manne,iliki na sukari.Niakavikoroga vizuri vyote kwa
pamoja.Chapati za maji wapo wanaopenda za chumvi,wengine sukari.Mie
napenda zote zote ila hizi zilikuwa za sukari.
Chapati za maji ni mlo rahisi sana kuandaa na fasta,najua kina dada na kina mama karibia wote mnaliweza.
Hapo chapati zipo tayari kuliwa.
Siku
sahau matunda tikiti,sasa hivi matunda yapo kibao hasa ya msimu.Kuna
mapapai,machungwa,embe,parachichi na matikiti.Tunda la msimu lisikose
kwenye kifungua kinywa au tengeneza juisi.
Hapo kifungua kinywa kikawa tayari viazi vya kukaanga,chapati za maji,chai ya maziwa na matunda.
N.B
Nipo kwenye maandalizi ya jarida la mapishi ya vyakula vilivyopo katika
mazingira yetu ya kila siku.Jarida hili limehusisha wanawake na wadada
waliopenda kushiriki kutoa ideas za mapishi yao wanayoyajua.Jarida hili
la kwanza litagusa kifungua kinywa tu namna ya kupika na namna ya
kupangilia huo mlo kwa kuzingatia mlo kamili wenye afya.Lengo hasa ni
kumpa mama/dada mawazo kuwa kuna uwanja mpana wa vyakula asikariri.Hata
dada wa kazi nyumbani linaweza kumsaidia pia.Mwisho wa mwaka ndio
utalipata,tena bure…stay tune
No comments:
Post a Comment