Sunday 19 August 2018

Mapambo ya mwilini


Ijapokuwa sura nzuri ya msichana inaweza kuvutia sana leo, wazee wa zamani walisisitiza juu ya kujipamba kwenye thamani kwa wanawake kuwa ni kujipamba kwa ndani [11]. Walitambua kuwepo kwa mapambo ya aina mbili kwa wanawake, yaani mapambo ya utu wa nje na mapambo ya utu wa ndani.
Mapambo ya mwili licha ya kupeleka ujumbe katika jamii juu ya nia na tabia ya aliyejipamba, pia yanahusiana na swala la afya ya mwili, roho na akili.Vitabu vya afya ya jamii ya mwili na roho, kwa miaka mingi vimetoa tahadhari katika maswala ya mapambo. Vimekemea kujichora kwa ‘tattoo’ na alama zingine mwilini [12]. Vitabu hivi imetambua kuwepo kwa mahusiano ya karibu kati ya mapambo na athari za afya ya mwili, roho na akili [13].
Baadhi ya rangi zinazotumika kuchora mapambo mwilini zinaweza kusababisha mzio, na vifaa vinavyotumiwa kuchora mapambo hayo vinaweza kusababisha uambukizo wa magonjwa yatokanayo na bakteria pamoja na virusi hatari kama vile virusi vya UKIMWI au virusi ninavyosababisha homa ya ini (Hepatitis B). Hii inaweza kutokea kutokana na kuchangia vifaa hivi na watu wengine. Lakini pia mapambo haya yanaweza kusababisha manundu ya ngozi (keloids) au kupata hisia ya kuungua mwili wakati wa uchunguzi wa kitabibu kwa kutumia mionzi ‘Magnetic Resonance Imaging’ (MRI).
Matatizo ya kisaikolojia pia hutokea pale mtindo wa kuchora katika ngozi unapopitwa na wakati na msichana akatamani kuondoa michoro hiyo bila mafanikio. Akili ya msichana inaendelea kukua na kupitia katika mabadiliko ya kimaamuzi kila mara na kutaka kwenda na wakati. Mitindo na mapambo mengi ya urembo hubadilika kulingana na mabadiliko ya kitamadini katika jamii yoyote ile.
Hina nyingi za madukani na dawa za kubadili rangi ya nywele, zina sumu ya para-phenylediamine (PPD) ambayo inaweza kusababisha mzio wa ngozi au mzio katika njia ya hewa. Katika baadhi ya nchi zilizoendelea mtu anapochora mwili wake kwa tattoo haruhusiwi kumwongezea mtu mwingine damu yake hadi mwaka mmoja upite baada ya kuweka michoro hii. Hii ni kutokana na hofu ya madhara ya kiafya anayoweza kupata wakati wa kuweka tattoo yasije ambukiza mtu mwingine
Athari zingine za mapambo ya mwili ni zile zinazosababishwa na kutoga masikio au pua. Kutoga masikio mara nyingi husababisha kuota manundu kwa baadhi ya wasichana na kupoteza dhana nzima ya urembo.Tatizo jingine liambatanalo na kutoga masikio au kuvaa hereni na vipini (vishaufu) puani ni kuchanika kwa matundu ya kuvalia vitu hivyo wakati yanapovutwa ghafla kwa bahati mbaya au wakati wa ajari. Baadhi ya vito na metali nyingi zinazotumika kutengeneza mapambo pia husababisha mzio wa ngozi kutokana na msuguano wa ngozi na vito hivyo kwa muda mrefu, jambo hili ni dhahili hasa kwa wale wanaovaa mikufu, bangili na pete.
Inashauriwa msichana au mwanamke asilale usiku akiwa amevaa hereni ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza kutokana na kuchanika kwa bahati mbaya kwa matundu ya masikio yake yanayotumika kuvalia hereni

Athari nyingine ya kijamii ambayao ni hasi inayotokana na urembo, hasa pale msichana anapojiremba kupita kiasi ni kukosa fursa za mafanikio. Waajiri wengine hasa wanawake, huogopa kumwajiri msichana au mwanamke anayejipamba na kujiremba sana kupita kiasi, hii ni kutokana na hofu kuwa wasichana wa namna hiyo huwa na nia ya kuwavutia kingono wanaume ikiwa ni pamoja na waume wa waajiri wao.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...