Sunday 19 August 2018

Afya ya miguu


Matunzo ya miguu kwa kutumia njia za asili au vipodozi vya kisasa pia yana umuhimu katika kuboresha afya ya miguu ya msichana na urembo wake. Katika kitabu chao kiitwacho “The Definitive Book of Body Language”, Allan Pease na Barbara Pease, wanasema kuwa miguu ni miongoni mwa sehemu za mwili zinazopeleka ujumbe wa mvuto wa msichana au mwanamke bila hata wenyewe kutambua.
Miguu isiyotunzwa vizuri inaweza kupoteza afya ya ngozi na kucha lakini pia inaweza kupasukapasuka. Msichana mwenye tatizo la miguu kupasuka au miguu isiyotunza vizuri huwa na doa katika urembo wake. Miguu inayopasuka inaweza kuchana mashuka, godoro na chandalua. Kama mipasuko ya miguu imeingia ndani sana inaweza kusababisha maumivu na mwonekano kama msichana amechanwa chanwa kwa wembe. Mipasuko ya miguu pia unaweza kusababisha uambukizo wa bakteria na kupata magonjwa hatari kama pepopunda (Tetanus) kwa urahisi.
Kwa ajili ya afya ya miguu na kuzuia mipasuko msichana anashauriwa kula chakula chenye asili ya mimea kama karoti, spinachi, maboga, viazi vitamu na samaki. Vyakula hivi huboresha afya ya miguu na ngozi kwa ujumla.Kwa afya kamili ya ngozi pia ni vema kunywa maji mengi kila siku na kuoga mara kwa mara. Kukabiliana na tatizo la miguu kupasuka na kuimarisha afya ya miguu, msichana anaweza kufanya mambo yafuatayo:-
• Loweka miguu inayopasuka kwenye maji ya uvuguvugu na yaliyoongezewa sabuni.
• Kisha loweka miguu kwa muda wa dakika 10 hadi 15 hivi kwenye mchanganyiko wa asali kikombe kimoja ndani ya galoni moja ya maji. Hii husaidia kuondoa ngozi iliyokufa na kuzuia damu kutoka katika mipasuko.
• Sugua miguu kila siku kwa jiwe laini ambalo halikwangui sana.
• Kausha miguu vizuri kwa taulo au kitambaa cha pamba hasa katikati ya vidole vya miguuni ili kuzuia kuvu na bakteria kuzaliana kwa urahisi miguuni.
• Paka mafuta, cream ya miguu au lotion yenye virutubisho kama vitamin E, siagi au Aloevera. Mafuta ya nazi au parachichi pia yanaweza kutumiwa kulainisha miguu. Vipodozi hivi vinaweza kutumiwa mara mbili, asubuhi na jioni kila siku.
• Usitumie wembe au kisu kuondoa mipasuko hii. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha mipasuko na madhara zaidi.
• Vaa soksi kila siku unapokwenda kulala wakati wa usiku. Msichana unaweza kuvaa soksi nyeupe kwa ajili ya kuzuia vumbi lisiingie ndani ya mipasuko ya miguu. Soksi nyeupe ni nzuri kwa vile hazitunzi joto jingi na kusababisha unyevunyevu miguuni.
• Dhibiti magonjwa au hali zinazochangia miguu kupasuka kama vile kukauka kwa ngozi (Xerosis); kuwa na uzito mkubwa, kusimama kwa muda mrefu, magonjwa ya ngozi kama vile mzio wa ngozi (Psoriasis na Eczema), ugonjwa wa kisukari na utendaji wa chini ya kiwango wa tezi la shingo.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...