Chukua unga wako wa karanga na
uuchanganye na asali mbichi kiasi kidogo, kisha acha kwa muda wa dakika
10 ili vichanganyike. Chukua mchanganyiko wako, kisha paka usoni hasa
zile sehemu unazoziona kuwa na mikunjo zaidi.
Subiri kwa dakika kama 10, kisha osha
uso wako na sabuni isiyo na kemikali baada ya hapo futa uso wako na
kitambaa kisafi na kikavu. Subiri tena kwa dakika 5 halafu paka mafuta
au losheni. Unashauriwa kufanya hivi mara moja kwa wiki.
Kiasili njia hii imekuwa ikitumiwa na
Wanyamwezi wa Tabora kama kipodozi kwa ajili ya mabinti wadogo pindi
wanapokaribia kufanyiwa sherehe maalum.
Unaweza pia kusugua taratibu uso kwa kutumia mchanganyiko wako ili
kuondoa takataka katika mwili wako ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo
unaweza kujipodoa kwa kupaka aina nyingine za vipodozi.
Kwa kazi hii ya ngozi, karanga zinazohitajika ni zile mbichi. Kitu
kinachohitajika ni kuchukua karanga mbichi ambazo hazijakaangwa kiasi
kidogo kama kikombe kidogo cha chai.
Zianike karanga juani kwa muda ili ziweze kumenyeka kwa urahisi bila
kukaanga. Saga karanga zako kwa kutumia blenda au kitu chochote
kitakachoweza kuzilainisha na kuwa unga laini.
No comments:
Post a Comment