Kuna kasumba ambayo imekuwa ikiwasumbua sana wanawake na wasichana,
mahali pengi duniani... kwa kupenda kuwa na makalio makubwa na wakidhani
wanaume wanapenda makalio makubwa, imefikia wakati wanawake wanajibinua
na wengine wanajipindisha utafikiri ni gari iliyokata center bolt yote
hiyo ni kutafuta shape ya mbinuko! Mtakuja kuvunja viuno bure!
Mbaya zaidi ni wale walioamua hata kununua dawa na vifaa vya kuongeza makalio. Napenda kusema kuwa kua
kama makalio yangekuwa dili basi wanawake woote wenye makalio
wangeolewa. mbona kuna wasichana wenye mbalazo kabisa (flat butts)
lakini wameolewa. Mtapata madhara kwa vitu ambavyo havina hata msingi,
mjifunze tu kuwa na tabia nzuri kila mwanaume ana kitu anachokipenda kwa
mwanamke. na si kwamba kila mwanaume anapenda kitu kilekile na isitoshe
mtu kushangaa ndo kwamba anapenda kumiliki ni sawa na ng'ombe wa
maonyesho watu wengi huenda kumuangalia kwa fahari ya acho na baada ya
hapo wanampotezea.
Jiamini wewe mwanadada na ujikubali vile ulivyo acha kuwa mcharuko!!
No comments:
Post a Comment