Thursday 15 November 2018

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na fair skin ila hizo areas ni korofi zenyewe ndo unakuta ngozi ni nyeusi inaboaje????Ila am sure unawaza kwanini una hilo tatizo i got you covered nimewasakia suluhisho ,Sababu kubwa ni ile constant rubbing of the thighs against each other(mapaja yakiwa yanagangana sijui nsemeje kiswahili kizuri au yanasuguana wakati unatembe ,tena inatokea sana kama mapaja yamekuwa makubwa ndo maana ile post ya wiki ilopita niliwawekea video ya kutoa mapaja makubwa sasa mapaja makubwa yanaenda sawa na ngozi yake kuwa nyeusi,pia kama ngozi ni kavu sana itasababisha weusi pia .
Nimesaka njia natural za kutoa weusi huu japo ziko za dukani .
1.ALOE VERA GEL
Tunajua wote jinsi Aloe Vera inatibu magonjwa mengi sana ,inazuia hadi cancer ,na ina contain subastances nyingi za kusaidia ku restore cells za ngozi yako,wanasema utapata results nzuri ukichanganya na Almond oil ambayo iko vizuri kwenye Vitamin E ,so chukua 2 table spoon ya Almond Oil na Aloe vera gel changanya massage sehem kuna weusi ,kama huna almond Oil tumia tu aloe vera yenyewe paka mapajani au kwapani acha kwa dakika 20 osha,kama wataka result haraka haraka paka daily .Paka na gloves ni chungu hii balaa.Howtoremovedarkskin (1)
2.BAKING SODA
Hii ni rahisi kila mtu anaweza kupata ,hii ina tabia ya ku exfoliate ngozi ,rinses the skin na huwa ina uproots dark and stained skin ,chakufanya ni mix baking soda na maji kuwa na uzito kidogo weka kwa sehem yenye tatizo iwe shingoni,kwapani au mapajani acha hadi ikauke then osha na maji ,fanya hivi kwa wiki mara mbili.Baking_Soda_Sodium_Bicarbonate
3.CUCUMBERS 
Hii vegetable ina contain powerful skin-lightening properties,ndo maana huwa wanaweka hadi kwenye macho mkienda for facial inasaidia toa weusi ule kwenye macho  ,ukitaka better results wanashauri u mix limao na matango.Matango pia yatafanya ngozi yako iwe smooth  na limao linasaidia kutoa zile blemishes/spots kwenye ngozi yako na huwa limao lina kama bleach flani hivi itakayosaidia kulighten ngozi yako sio kukuchubua inang’aa tu na weusi utapungua.
Cucumber on a white background
4.LIMAO
Limao liko rich in Vitamin C na antioxidants ambayo inazifanya ziwe effective kwenye kutoa cells ,pia zina uwezo wa  accelerate the regrowth of healthy skin cells (skin cells zitakuwa nyingine ambazo ni healthy zile zilizokufa zikishatolewa),limao inasaidia pia ku tone ngozi yako.Paka juice ya limao kwenye area zenye tatizo hilo acha kwa dakika 20 osha then kama una mafuta paka .Waweza ongeza na asali kwa limao upake kwa pamoja na kurub kwenye mapaja yako/shongoni/kwapani.lemon
5.COCONUT OIL WITH LEMON JUICE 
Hapa kinachofanyika ni kuwa mafuta ya nazi ni mazuri sana kwa ku mosturize ngozi yako ambayo ni kavu na pia ku lighten ngozi yako wakati limao tumesema lina blemishes ngozi yako maana lina virtue ya bleaching.So mix juice kidogo ya lmao na matone au kijiko cha mafuta ya nazi inategemea na wingi unaotengeneza ,massage kwa dakika 15 ,futa na nguo kavu then osha na maji ya vugu vugu.0b344a5e326bdbcad1500c12f43d62f6

6.SUGAR,ASALI NA LIMAO

Sukari ni nzuri sana kwa ku exfoliate ngozi yako ila si nzuri kuila tu maunene.com  itasaidia pia ngozi yako kutoa zile dead skin cells ,asali ni natural moisturizer ,mix  1 teaspoon of sugar na 1 tablespoon ya asali kwenye juice ya limao ,apply it kwa ku rub gently in i a circular motion baada ya hapo osha na maji ikishakaa dakika10 .Si mwajua kuna watu wanafanya scrub ya sukari .Howtoremovedarkskin (3)

Mkumbuke kuwa hizi ni natural remedies so ukisikia neno bleaching au skin lightening ni kidogo sana na unataka kutoa weusi kufanya ngozi irudi kwa rangi yake ,sio kwa kiasi kile cha cream msichanganye madesa 

Mix and Match Mishono styles

Yes hii style imerudi tena kwa kasi ,sio kwamba iliondoka ila fashion girls waliipumzisha kwa muda,but now kila mtu ana rock mix and match.
Vitenge viko bold kwa colors na maua yake so cha muhim cha kuzingatia sana wakati unataka kushona style hii ya ku mix and match hakikisha kwamba kuna foundation color inayopatikana kwenye vitenge vyote viwili bila hivyo utaonekana kama una bustani kichwani.

shorts and shirt 
wrap style
i love this dress 
another look i love 
jumpsuit .

Wednesday 14 November 2018

MISHONO YA VITENGE 2018

wadau wanawake wote kwa ujumla.Mtafute fundi wako alipo alafu mpekazi mambo ya copy, paste na editing pia inaruhusiwa.
Embu jichagulie jishono lako hapo yani kwa raha zako mwanamke.









MISHONO YA VITAMBAA 2018 VYA SATINI

huwa tunakuletea Mishono mbalimbali ya nguo,leo tuna mishono ya lace ,vitenge na satin.Naomba kuiita hii peplum new level wengine waita peplum ya visu mana mshono wa chini ni wa mikato flani ya visu.African Print  imemixiwa na Fringe.tunatupia Mishono mikali ilokiki kwa wiki nzima huko mitandaoni











#TBT :: Noel Ndale’s Obsession With Kanzu

Tuna throwback from post ya July 8 mwaka 2016
Nahisi Noel is obsessed with Kanzu kwa kuangalia tu many times ameweva kutinga kanzu utaona his love for this attire,Napenda anavyoa add his own touch kwenye mionekano yake ya kanzu.Its Friday na ni perfect for this look,hope utakuwa inspired na wewe next week Insha Allah utinge hivi ukasali.Noel Ndale (6)
Kanzu with Kimono ,kilemba and mirrored sunglassesNoel Ndale (7)
such a clean white and blue lookNoel Ndale (8)
He used a beret hat instead of Baraka shee for this look,do you like ???
Noel Ndale (1)
Another Blue kanzu with just kilemba ,this time alitupia tu kilemba hakufungaNoel Ndale
Rock Kanzu with a blazer
Noel NdaleNoel Ndale (5)
Kipindi cha Ramadan pia alivaa sana Kanzu ,hapa ilikuwa mualiko wa Iftar Noel Ndale (2)
Love this look simple and stylishNoel Ndale (4)
He rocks kanzu with sneakers wakati most of you mnavaa na sandals,well ina depend pia na unapoenda au ulipo
Noel Ndale (3)
Hapa ni just a beige/brown Kanzu hakukua na acessories zingine zaidi ya Viatu na saa

Tuesday 13 November 2018

Zijue mbinu Za kujitibu chunusi Bila Kutumia Na Gharama Kubwa

Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso, kifuani na hata mgongoni. Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani bakteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris. Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.

Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe (adolescents).

Hivyo zifuatazo ni mbinu za kujitibu chunusi;

1.   Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.

Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

 2. Limao
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.

3. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanya kazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10. Lakini pia safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

 4. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.

Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

5. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10 hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

6. Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha mpaka asubuhi.

MHIMU: Kunywa maji ya kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe na mazoezi ya viungo na ujiweke msafi kila mara.

Njia hizi za Asili zinaweza kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha. Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.

Mambo yafuatayo husaidia nywele kuwa na afya njema

1. Kula chakula bora chenye matunda, nafaka na mboga kwa wingi pamoja na mbegu za alizeti.
2. Kunywa maji ya kutosha pamoja na maji ya matunda (juisi) ya asili ambayo haijasindikwa viwandani.
3. Kufanya mazoezi ya mwili kila siku.
4. Kupunguza nywele kwa kuzinyoa kila baada ya majuma manne hadi matano hata kama zinafugwa ili ziwe ndefu.
5. Usikae kwenye jua kali kwa muda mrefu au vaa kofia uwapo juani ili kuzuia mionzi ya jua (ultraviolet radiations) isidhuru nywele.
6. Usioge maji yenye chumvi na safisha nywele kwa maji yasiyokuwa na chumvi mara baada ya kuogelea katika maji yenye chumvi. Maji chumvi yana alkaline ambayo inaharibu keratini ndani ya nywele
7. Usikaushe nywele kwa joto kali. Joto kali la ‘dryer’ na vifaa vingine vya kutengenezea mitindo ya nywele huharibu keratin ya nywele. Ni vema joto likawa la wastani na kwa muda mfupi.
8. Kausha nywele kwa taulo kwanza kabla ya kuchana nywele zenye umajimaji kwa nguvu. Tumia chanuo yenye nafasi pana katika meno yake.
9. Kama nywele zinakaukiana vibaya zitibu kwa kupaka mchanganyiko wa ute wa yai na asali kijiko kimoja au mchanganyiko wa ndizi mbivu na asali kijiko kimoja kisha paka kwenye nywele kwa muda wa dakika 30-40. Hakikisha kuwa mchanganyiko huo unaifiki ngozi ya kichwa vizuri na uache kichwani kwa dakika 40 kabla ya kuondosha kwa kuosha nywele kwa maji ya uvuguvugu au maji ya limao.
10. Kupaka mafuta ya nazi yenye uvuguvugu yaliyochanganywa na maji ya limao kila siku huzifanya nywele kuwa na afya nzuri.
11. Baada ya kupaka mafuta ya nazi vizuri kichwani funika nywele kwa kitambaa chenye uvuguvugu ili mafuta yapenye ndani ya vinyweleo vya nywele kwenye ngozi ya kichwa.
12. Kumbuka kusafisha nywele mara kwa mara husaidia kupunguza tatizo la ugonjwa wa mba kichwani na kupunguza muwasho wa ngozi ya kichwa. Inashauriwa kutochanganya aina mbalimbali za vipodozi vya nywele kinyume na maelekezo ya watengenezaji.Ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara ya vipodozi vya nywele ni busara kujaribu kiasi kidogo kwenye ngozi ya sikio na kuiacha kwa siku nzima bila kusafisha kwa maji ili kuona kama itasababisha muwasho au kuvimba kwa ngozi.
Ofa! Ofa! Ofa!
Ni jarida la SMS Bomba za vichekesho!
Jipatie 📕Kitabu cha Vichekesho Vikuu Vikali 300+✔ kwa bei ya ofa ya Tsh 2500/= tuu kwa leo!, kutoka bei yake ya kawaida ya Tsh 6500/=.
<<<Bofya hapa kujua zaidi>>>

Tatizo la mvi wakati wa usichana

Mtu yeyote anayeota mvi kabla ya kufikisha miaka 35 ya umri wake, huwa anakabiliwa na tatizo la kuota mvi kabla ya wakati wake (premature graying). Ingawa tatizo hili mara nyingi hutokana na urithi wa vinasaba vyenye mwelekeo wa kuota mvi kabla ya wakati wake, lakini mambo yafuatayo pia huchangia:-
(1) Kukosa hali ya usawaziko sawia wa vichocheo vya mwilini.
(2) Matumizi makubwa ya muda mrefu ya dawa zenye kemikali.
(3) Uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe kwa kiasi kikubwa.
(4) Kula vyakula vyenye acid nyingi kila siku.
Wasichana wengi wanaokabiliwa na tatizo hili hupata msongo wa mawazo kutokana na mwonekano wa kizee wa nywele zao licha ya ukweli wanaojua kuwa wao siyo wazee. Kuwa na mvi mapema hakumaanishi kuwa mtu amezeeka ila ni kunaonyesha kuwa mwili wa mtu huyo hauzalishi malemin ya kutosha katika vifuko vya nywele za kichwani.

Tatizo la ndevu kwa wasichana

Wasichana wanapoota ndevu nyingi hukabiliwa na changamoto za kisaikolojia na ulimbwende. Mitazamo na mila nyingi za kijamii katika bara la Afrika, bado zinakumbatia unyanyapaa wa wazi au wa kificho kwa wasichana wanaoota ndevu nyingi. Msichana mwenye ndevu nyingi anavuta hisia na macho ya wanaume na wanawake wenzake pia kiasi kwamba anatazamwa kwa namna ambayo wakati mwingine inamnyima raha. Wakati mwingine wanaume hawapendi kuoa wasichana wenye ndevu nyingi kutokana na mwonekano unawafanya wasichana hao kuwa kama wanaume.
Katika hali ya kawaida msichana anatazamiwa asiwe na nywele nyingi kwenye kidevu, juu ya mdomo wake, kifuani, tumboni na mgongoni. Na hata akiwa nazo basi ziwe malaika zisizokuwa na rangi nyeusi iliyokolea na kuwa ngumu kama za wanaume.
Mwanamke anapokuwa na nywele nyingi sehemu hizo humaanisha kuwepo kwa hitilafu za kijenetiki au dosari za ulinganifu wa vichocheo vya jinsia mwilini mwake. Wasichana wengine maumbile yao yanayotokana na vinasaba yanawafanya wawe na nywele nyingi mwilini, hali hii kitabibu hujulikana kama ‘hypertrichosis’.Dosari za ulinganifu wa vichocheo vya kijinsia kwa wasichana zinaweza kusababishwa na:-
(1) Kuzalishwa kwa wingi kwa vichocheo vya ujinsia toka katika mifuko ya mayai.
(2) Uvimbe katika mifuko ya mayai (ovarian tumors)
(3) Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango zenye vichocheo pia zinaweza kuwa chanzo cha tatizo hili kwa baadhi ya wasichana. Dawa hizi husababisha ongezeko la vichocheo bandia vya ujinsia kuwa vingi katika mwili wa msichana.
(4) Matumizi ya dawa na vipodozi vyenye viambato vya dawa kama testosterone na steroid zingine pia husababisha tatizo hili endapo dawa hizi zitatumiwa kwa muda mrefu.
(5) Uvimbe wa tezi ya Adrenali iliyo juu ya figo pia unaweza kusababisha tatizo hili.
(6) Unene wa kupindukia (obesity) kwa wasichana pia unaweza kusababisha ongezeko la kichocheo cha kiume (Androgen) mwilini mwa msichana kutokana na nyama zenye mafuta mengi kugeuza kichocheo cha kike cha estrogen kuwa kichocheo cha kiume cha androgen. Androgen inapokuwa nyingi mwilini husababisha msichana kuwa na tabia za kiume ikiwa ni pamoja na kuota ndevu na kuwa na sauti nzito.
(7) Matumizi makubwa na holela ya baadhi ya dawa zenye kemikali kama vile Danazol, Cyclosporin na zingine pia husababisha tatizo hili.Ni vizuri kwa wasichana kuepuka matumizi ya dawa bila kupata ushauri wa kitabibu.
(8) Ikumbukwe kuwa wakati mwingine kunakuwepo na hali ya ulinganifu wa vichocheo vya ujinsia mwilini kama kawaida, lakini tatizo likawa ni mwitikio wa hali ya juu wa nywele (oversensitivity) kwa kiasi cha kawaida cha kichocheo cha kiume kilichoko mwilini mwa msichana (androgen).Katika hali hii, msichana pia anaweza kuwa na nywele nyingi mwilini kuliko kawaida.

Dalili zinazo ambatana na kuota ndevu kwa msichana

• Kuota chunusi nyingi.
• Kutokupata damu ya hedhi kama kawaida. Wakati mwingine msichana hupata damu pungufu sana, kutoiona kabisa au kupata hedhi yake bila mpangilio maalumu.
• Matatizo mengine yanayosababisha ndevu kuota kwa wingi pia yanaweza kusababisha ugumba (kushindwa kupata ujauzito na kuzaa watoto).
• Kusinyaa kwa matiti na mfuko wa mji wa mimba.
• Kututumuka na kunenepa kwa kinembe kuliko kawaida (enlargement of the clitoris).
• Kuwa na sauti nzito na wakati mwingine kisanduku cha sauti (Adam’s apple) hunenepa kama cha wanaume.
• Mtawanyiko wa nywele mwilini huwa kama wa kiume, pamoja na ndevu msichana huota nywele kifuani, tumboni, mapajani, mgongoni, miguuni na mikononi kwa wingi. Wengine pia huota nywele nyingi kwenye makalio na kuzunguka sehemu ya njia ya haja kubwa na hali hii ya msichana kuwa na  nywele nyingi mwilini, hujulikana kama “hirsutism”.
Ofa! Ofa! Ofa!
Ni jarida la SMS Bomba za vichekesho!
Jipatie 📕Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga🌿🍅 kwa bei ya ofa ya Tsh 2500/= tuu kwa leo!, kutoka bei yake ya kawaida ya Tsh 7000/=.
<<<Bofya hapa kujua zaidi>>>

Jinsi msichana anavyoweza kukabiliana na tatizo la ndevu

• Kwanza kabisa msichana anatakiwa kuelewa kuwa kuota ndevu sio dhambi na wala si kosa, hivyo basi ndevu zisiwe chanzo cha msongo wa mawazo.
• Msichana asiache ndevu zikawa ndefu kama za wanaume kwani zinavuta hisia za watu kumwangalia angalia kiasi kwamba zinaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia. Ndevu zikatwe na kuwa fupi kadri inavyowezekana kwa wakati wote. Mkasi au cream ya kuondoa nywele inaweza kutumika kwa lengo hili. Ile dhana ya wanawake wengi kwamba ndevu zikinyolewa zinaongezeka maradufu haina ukweli wowote wa kisayansi.
• Ni bora wasichana wakajiepusha na matumizi ya vipodozi vyenye viambato vyenye dawa za magonjwa ya ngozi.
• Ndevu zising’olewe kwa vidole, hii inaweza kusababisha uambukizo wa bakteria katika ngozi kwa urahisi na kuleta matatizo ya kiafya.
• Wasichana waepuke matumizi ya dawa zenye steroid bila kupata ushauri wa kitaalamu toka kwa wahudumu wa afya na maswala ya tiba.
• Kufanya mazoezi ya mwili na kudhibiti unene wa mwili pia husaidia katika udhibiti wa tatizo hili.
• Endapo nywele zimetapakaa kwa wingi miguuni na mikononi na kuleta muonekano wa kiume ni bora kuvaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri ili kuepuka msongo wa kisaikolojia ambao unaweza kutokea kutokana na mtazamo hasi wa kijamii.
• Wakati wote jivunie kuwa msichana, usikubali kitu chochote kikuondolee hisia zako za kuwa msichana kamili. Afya ya mwili na roho huanza na afya ya akili. Jitambue, jipende, jiheshimu na jiamini kwani wewe ni msichana kama walivyo wasichana wengine.
🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (UREMBO NA MAVAZI YA MSICHANA).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔
Mtafute ndugu yako hapa Na yeye anakutafuta sana
👉

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...