Tuesday 13 November 2018

Athari za kiafya kutokana na kope za bandia


Urembo kwa kutumia kope za bandia siku hizi unaonekana kushamili miongoni mwa wasichana na wanawake wengi. Jambo hili licha ya kuwa na uwezekano mkubwa wa kusababisha madhara makubwa katika afya ya macho, wasichana wengi wanalishabikia.
Miongoni mwa madhara ya kiafya kutokana na urembo huu ni pamoja na upofu, uvimbe wa ngozi laini inayofunika macho, muwasho wa macho, mzio utokanao na gundi ya kubandikia kope bandia kama vile super glue na gundi zingine zenye sumu ya formaldehyde. Madhara mengine ya kope bandia ni uambukizo wa bakteria, kuvu (fungus), virusi na parasaiti. Matumizi ya kope bandia katika urembo, pia yanaweza kusababisha vumbi kuingia machoni na kusababisha muwasho na uvimbe wa macho.
Lakini pia kope zinaweza kujiachia hasa wakati wa usingizi na kuingia machoni. Hii hutokea zaidi kwa kope bandia za muda mfupi (temporary fake eyelashes) ambazo zinakusudiwa kuvaliwa kwa muda usiozidi saa 24. Kope za namna hii, haziwezi kukabiliana na misukosuko wakati wa usingizi, kuogelea au kuoga.
Matatizo mengine ya kope za bandia ni pamoja na kusababisha kope za asili kuharibika na kunyofoka (traction alopecia) au kuota kwa nyusi zinazopindia ndani (endotropion) na kudhuru afya ya macho.
Hali hii hutokea zaidi pale msichana anapotumia kope bandia zinazokaa kwa muda mrefu (semi-permanent artificial eyelashes). Kope hizi kugundishwa kwenye kope za asili na kushikizwa kwenye kope moja moja kwa muda wa zaidi ya saa mbili. Kope za muda mrefu ni ngumu kuzitoa kwa vile hushikizwa kwa gundi kali.
Katika gazeti la Risasi (ISSN 0856-7999, Na.1062) la Jumamosi November 23-26, 2013 linalochapishwa na kampuni ya Global Publishers LTD –Tanzania, kulichapishwa habari ya mrembo mmoja wa jijini Dar-es-Salaam aliyepata upofu wa macho kutokana na urembo wa kubandika kope za bandia.
Dada huyu aliyepatwa na athari hii mbaya ya urembo alisema kwa kwa majonzi makubwa maneno yafuatayo “Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza…macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini”. Inasadikika kuwa gundi iliyotumika kubadika kope bandia katika macho ya mrembo huyu ni gundi ya super glue. Ukweli ni kwamba thamani ya afya ya macho ni kubwa kuliko faida ya urembo.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...