Thursday, 9 August 2018

Supu ya ng´ombe na mbogamboga


Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 45
Muda jumla; lisaa 1

Mahitaji



500g/ nusu kilo nyama ya supu
Karoti 1 kubwa
Kintunguu maji 1 kikubwa
Hoho nusu mara 3 (ukipenda rangi tofauti; kijani, njano, nyekundu)
Vijiko 2 beef bouillon powder au beef cubes 2
Viazi 3 vya wastani
½ kijiko cha chai tangawizi ya unga
Chumvi kwa kuonja ikihitajika
Maji lita 1.5

Maelekezo

Katakata nyama vipande vidogovidogo



Osha nyama, weka pembeni



Andaa mbogamboga; katakata viazi, karoti, kitunguu maji, hoho na giligilani, weka pembeni



Kwenye sufuria katika moto wa wastani, weka nyama, maji lita 1, beef bouillon powder/ beef cubes, kitunguu maji na tangawizi ya unga



Funika na mfuniko, acha ichemke kwa dakika kama 30 au mpaka nyama ilainike. Endapo maji yatakauka kabla nyama ilainike, ongeza maji zaidi



Pika mpaka maji yakikarikia kukauka na nyama ikishalainika



Ongeza viazi na karoti kwenye nyama



Acha viive pamoja mpaka maji yakauke kabisa



Weka hoho



Kaanga kwa dakika moja hadi 2



Ongeza maji kiasi unachohitaji kwa supu. Funika na mfuniko tena, acha ichemke kwa dakika chache



Ongeza giligilani na chumvi kama itahitajika



Kula ikiwa ya moto



Enjoy

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...