Saturday, 18 August 2018

Jinsi Asali, Sukari, Maziwa, na Limao vinavyoweza kuleta Mng`ao mpya katika Sura yako

Usafi wa  uso ni moja ya mambo muhimu sana kwa mwanamke au mwanaume yeyote  yule ambaye anapenda kuwa nadhifu na mwenye mvuto. Kumbuka “reception  ndio kila kitu “. Unapokutana na mtu sura yako na mwonekano wa sura yako ndio kitu cha kwanza kinachomtambulisha kwamba wewe ni nani  na upo kwenye hali gani.

Kuna njia nyingi za kuufanya uso wako uvutie na kupendeza. Leo tutaongelea zaidi jinsi ya kusafisha uso kwa njia ya asili.  Mie hupenda kutumia njia ya asili sababu ni rahisi kupata vifaa na ni nafuu . Pia mtu anaweza kufanya kwa mazingira yoyote yale. Na matumizi ya vitu vya asili kwenye mwili husaidia kupunguza sumu mwilini kwani kutumia vipodozi vyenye kemikali husababisha miili yetu kujaaa sumu.

Njia ya asili ya kusafisha na kupendezesha mwili ninayokueleza leo inahitaji vitu vikuu vinne : asali, sukari, maziwa, na limao.

Haijalishi aina gani ya ngozi unayo , njia hii ya asili inaweza kutumika kwa aina yoyote ile ya ngozi iwe ngozi yenye mafuta au ngozi kavu.

Kiasi cha mahitaji yanayohitajika:

  • Kijiko kimoja cha asali
  • Kijiko kimoja cha sukari
  • Kijiko kimoja cha maziwa
  • Kijiko kimoja cha limao


Utaratibu wa kusafisha uso
Weka  mahitaji hapo juu kwenye chombo kilicho kisafi, changanya vitu vyako mpaka vilainike, viache kwa muda wa dakika 10 ili viweze kuchanganyikana vizuri na  na sukari iweze kuyayuka vizuri.

Baada ya mchanganyiko wako kuwa tayari  chukua kipande cha pamba kilicho kisafi tumia kupakia mchanganyiko wako usoni . Na kumbuka ni vizuri uso ukiwa mchafu  na upaswi kuosha uso alafu ufanye  zoezi hili. Baada ya kupaka mchanganyiko wako usoni  kaa kwa dk 15 .

Baada ya hapo chukua maji ya uvuguvugu, kitaulo kisafi na sabuni ya kipande “vizuri kutumia sabuni ya kipande maana haina kemikali nyingi” tumia kitambaa  kuoshea uso wako pamoja na sabuni.

Basi baada ya hapo umekuwa umemaliza zoezi lako la usafi wa ngozi yako
Kumbuka njia hii aina madhara yoyote na haibadilishi rangi au muonekano wa ngozi yako na unashauliwa kufanya mara kwa mara  ili kukupa mvuto zaidi.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...