Tuesday 31 July 2018

HAYA NDIO MADHARA KUMI YA SIMU KIAFYA..



ulimwengu wa teknolojia unakua kwa kasi sana, mwaka 2005 na kurudi nyuma simu za mkononi zilikua chache sana lakini pia kabla ya mwaka 2000 simu hizi zilikua hazipo kabisa na watu wengi walikua wanatumia simu za mezani,barua au simu za posta kufanya mawasiliano...
lakini leo hii mfumo wa maisha umebadilika kabisa kiasi kwamba simu imekua moja ya vitu vya msingi sana vya binadamu ukiachana na chakula, nguo na maradhi yaani ukiwa huna simu kwa sasa mambo mengi na huduma nyingi huwezi kupata kirahisi ikiwemo huduma za kifedha na malipo ya huduma mbalimbali ka luku, maji, na kadhalika..

 lakini kama ilivyo ada kila kizuri kinachokuja au kila teknolojia mpya huambatana na madhara yake, tafiti zinaonyesha kuna magonjwa au matatizo hayakuwahi kuwepo kabisa kabla ya teknolojia kuanza lakini leo ndio yamezidi zaidi baada ya teknolojia kushika kasi.
hebu tuone madhara makubwa yaliyojificha nyuma ya simu za mkononi

saratani za ubongo;
 kitaalamu simu hutumia mionzi ya radio frequency au non ionizing radiations ambazo kimsingi hazina madhara makubwa sana kama ionizing radiation kama x ray na wenzake lakini mionzi hii ambayo hutolewa na simu kwenye antena zake tafiti zimeonyesha kwamba matumizi yake hasa yakiwa makubwa sana hasa kwa wale waongeaji wakubwa wa simu husababisha baadhi ya kansa za ubongo.

ugumba na utasa;
 tafiti moja iliwahi kufanyika na kugundua kwamba matumizi ya mionzi ya simu maarufu kama wi-fi yanashusha sana kiwango cha mbegu za kiume kwenye korodani ukilinganisha na wanaume ambao hawatumii wi-fi kwenye kazi zao, tafiti hizi zilifanyika baada ya kuona ongezeko kubwa la wanaume tasa kwenye jamii yetu na moja ya majibu ilikua ni matumizi ya wi-fi.

magonjwa ya kuambukiza;
 daktari mmmoja bingwa mtaalamu wa wadudu kitaalamu kama microbiologist alifanya tafiti na kugundua kwamba simu tunazotembea nazo sababu ya shughuli mbalimbali tuzazofanya tukiwa nazo huwa zina wadudu wengi wa maradhi kuliko wadudu wanaopatikana pembeni ya choo, tafiti iliongeza kwamba moja ya bacteria waliopatikana ni wale wasiosikia dawa kabisa mfano e.coli na kutoa ushauri watu kusafisha simu zao na dawa za kuua wadudu yaani antseptic angalau mara moja kwa siku kwani kutumia simu na baadae kula bila kunawa vizuri unakula uchafu mwingi sana.

aleji mbalimbali;
 kuna watu wengi wamekua wakiugua magonjwa ya ngozi kwa kuvimba na kuwashwa bila kujua chanzo ni nini lakini wataalamu wamegundua kwamba madini ya nickel yanayopatikana kwenye simu ni moja ya vyanzo vikuu vya aleji na mtu anaweza kuteseka miaka mingi bila kujua chanzo.

kukosa usingizi na msongo wa mawazo;
 watu wengi wamekua wakitumia simu mpaka usiku sana wakiwa kwenye mitandao ya kijamii hii huharibu mfumo wa usingizi na kujikuta mtu analala masaa machache sana na kuamka kwa kuchelewa sana au kuamka mapema kuwahi kwenye shughuli zake, na huko kazini hujikuta akilala muda mwingi na kupoteza ufanisi na kupelekea msongo wa mawazo.

mazoea au addiction;
 huko china wameanzisha clinic za kutibu wagonjwa ambao wamepata addiction ya kutumia internet ya simu na kushinda kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kua unaona msihara lakini siku hizi watu hawawezi kukaa nusu saa bila kuangalia kwenye simu na mtu simu yake ikikosa intaneti masaa kadhaa hukosa raha hata kama hakuna kitu cha msingi anafuatilia huko, kifupi ni kwamba watu hawa huko china wanatibiwa kama wahanga wa madawa ya kulevya.

matatizo ya macho;
 simu ina kioo kidogo sana ukilinganisha na kile cha komputa hivyo mtu hulazimika kukaza macho sana ili aweze kuona vizuri na mara nyingi watu wakitaka kulala baada ya kuzima taa huendelea kutumia simu na kupata mwanga wa moja kwa moja kutoka kwenye simu na hii huharibu uwezo wa macho kufanya kazi na baadae mtu atalazimika kuvaa miwani.

maumivu makali ya mgongo;
 matumizi ya simu huhitaji muhusika kuinama muda mwingi hasa kama anatuma meseji ili aweze kuona vizuri, lakini aina hii ya mkao humfanya mtumiaji kupindisha mgongo na kuanzisha maumivu makala sana ya mgongo hapo baadae.

kuvunjika kwa mahusiano;
 simu zimekua zikivunja mahusiano ya kijamii na mahusiano ya kimapenzi yaani watu wawili wanaweza kusafiri mkoa mmoja mpaka mwingine bila kufahamiana kiundani na hii inaweza kukunyima fursa kwani hujui unasafiri na nani huenda akikusaidia kuboresha maisha yako lakini pia simu ndio zimekua chachu ya watu kutembea nje ya ndoa zao au nje ya mahusiano yao na kuficha siri huko.

ajali mbalimbali;
tafiti zimeonyesha kupungua sana kwa umakini kwa madereva wanaotumia vyombo vya moto huku wanatumia simu lakini pia hata watembea kwa mguu wanaotembea huku wanatuama meseji wanakua kwenye hatari kubwa ya kuumia na kupata majeraha...hii imesababisha ajali nyingi sehemu mbalimbali na baadhi ya miili iliokotwa simu zao zikionyesha walikua wanatuma meseji, naomba nikazie hapa...unaweza kua unafikiri unatuma meseji mara moja tu lakini sekunde moja tu inaweza kukuokoa au kukuua ukiwa barabarani.

mwisho;
 kwa madhara niliyotaja hapo juu nafikiri ni wakati wa wewe ndugu msomaji kuanza kuchukua hatua na kutumia simu hizi pale unapokua unahitaji kweli hii itakusaidia kukulinda na majanga mbalimbali yatokanayo na simu

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...