Friday 13 July 2018

DALILI ZA NDOA ILIYOKUFA

Kuna mambo mengi ambayo hupelekea ndoa kufa,leo nitazungumzia dalili chache zinazo onyesha ndoa kuelekea kufa.

Alichokipanga Mungu  mwanadamu si rahisi kupangua.

 Wanandoa wanaposhindwa kutatua migogoro yao wenyewe.
Mwanandoa anapodhani anaweza kuishi mwenyewe bila mwenza wake.
Wanandoa wanapoona kuwa watoto ndiyo sababu pekee inayowafanya kuendelea kuwa katika ndoa.
Wanandoa wanapoanza kuogombana ndani ya ndoa,yaani kila mmoja anahofu kujadiliana na mwenzi wake masuala yanayo wahusu.
Pale  mwanandoa unapogundua kuwa ndani ya ndoa kuna mambo mengi mabaya yanayofanyika kuliko mazuri.
Wakati mwingine unaona mwenzi wako hakushirikishi masuala muhimu mpaka hatua ya mwisho unapogundua mwenyewe.
Kugombana kwa suala moja kila wakati.
Wakati mwingine mmoja wenu au wote mnapokosa hamu ya tendo la ndoa.
Kupata uzito katika mawasiliano unapotaka kuwasiliana na mwenzi wako.Mume au Mke.
Heshima aliyokuwa anakupa mke/mme mbele za watu inapopungua.Kama yote haya yatafanyika kinyume kwa kuyaweka katika hali yenye faida basi ndoa inaweza kudumu zaidi.Usisite kutoa maoni yako hapo chini kama umevutiwa na makala hii.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...