Sababu ya ngozi kuwa na mafuta hutokana na na tezi za sebaceous na
kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango ambacho ambacho kinatakiwa. Lakini
licha ya tezi hizo aina za sebaceous kuzalisha kiwango cha mafuta kwa
wingi, zipo pia sababu nyingine ambazo zinafanya ngozi kuwa na mafuta
ambazo kama ifuatavyo.
- • Kurithi.
- • Lishe.
- • Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
- • Ujauzito.
- • Baadhi ya vipodozi .
- • mabadiliko ya hali ya hewa hasa joto.
Na madhara ambayo yanatokana na ngozi yenye mafuta ni kwamba, ngozi
huweza kutengeneza ngozi yenye tabaka lisiloisha vipele pamoja na
chunusi kwa muda mrefu.
Baada ya kuona baadhi ya sababu na athari ya ngozi kuwa mafuta, sasa tuangalie namna ya kutunza ngozi zenye mafuta:
1. Ngozi yenye mafuta
inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia
vinyweleo visizibwe na mafuta. Lakini Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako
na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au mara tatu kwa
siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta
zaidi.
3. Epuka kutumia vipodozi
ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha
sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba
vinyweleo na kupelekea kutokea kwa chunusi ambazo zitaufanya mwili kuwa
na mafuta.
4. Chagua kile
unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa
vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida
zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni
zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini
mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye
alkoholi.
5. Lakini pia unashauriwa ya kwamba hakikisha unatumia mafuta ambayo yametengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.
Endapo utayazingatia hayo mwili wako utakwenda kuwa katika hali ya ubora zaidi, na kufurahia ngozi isiyo na kasoro.
No comments:
Post a Comment