Saturday, 26 August 2017

NJIA YA ASILI KUTIBU NGOZI YENYE PIGMENTI/GET RID OF HYPER-PIGMENTATION NATURALLY.


Hyper-pigmentation/Pigmenti ni vile ngozi inatokewa na alama kama kovu, inakuwa rangi darker kuliko rangi asili ya ngozi yako. Wengi hutokewa hii baada ya kupata vichunusi/acne unavyotoboa na ile inayokaa kwa muda bila kutibiwa. Na wengine hutokewa hii baada ya kujifungua.






Inaweza kupunguzwa kwa kula vyakula vyenye anti-inflammation kama vile nyanya, samaki, kutumia  olive oil nk.

Kabla ya kuenda kwenye hizo njia unazopaswa kutumia, hiziz ni few tips unazotakiwa kuzifuata::

  • Kunywa maji ya kutosha ili ngozi yako iwe hydrated na isikakamae, kunywa green juices na maji fresh ya nazi.
  • Fanya Exfoliation mara 2 kwa wiki, ili kuondoa ngozi iliyokufa.
  • Kuwa na subira..Patience! sio unaanza wiki 2 tu unaona hamna mabadiliko then unakimbilia madawa makali, mwisho wake unaishia kujichubua.
  • Usitoboe wala kukuna hivyo vichunusi/acne itazidisha tu.


Njia asili za kutibu Ngozi yanye Pigment/Hyper-pigmentation::
Tumia Tumeric face mask/Binzari manjano.

Binzari manjano inasaidia kupunguza chunusi na ina lighten huo weusi wa pigmenti usoni. Hivyo unaweza kuongeza binzari manjano kwenye face mask yako unayotumia (kama huwa unatengeneza mwenyewe) angalau mara 2 au 3 kwa wiki. BonyezaHAPA kuona Jinsi ya kutengeneza Tumeric face mask.

Tumia Ndimu/Lemon.

Ndimu inatumika sana katika kufanya ngozi iwe lighter, hivyo unaweza tumia ndimu kupunguza ule weusi polepole hadi uishe. Chukua ndimu iliyokatwa then paka sehemu kwenye huo weusi, acha hiyo juice ya ndimu ika kwa muda wa dakika 10 the nawa uso, paka moisturizer. 

Kama ngozi yako ipo sensitive sana basi changanya ndimu na asali au aloe vera gel ndio upake. USIPAKE NDIMU KWENYE NGOZI ILIYOCHANIKA/CHUBUKA!

Tumia fresh Aloe Vera gel.

Aloe Vera gel pia inatumika katika vitu vingi sana, inasaidia kulainisha ngozi na hata kuondoa alama. Unaweza kupaka Aloe Vera gel na ukakaa nayo siku nzima bila kunawa, wengine huwa wanapaka kama moisturizer, wanapaka kabla ya kupaka makeup. Hakikisha tu unatumia Aloe Vera gel amabayo ni fresh.


Tumia Rhassoul Clay/ Udongo kutoka Morocco.

Inasmekana kuwa huu udongo una healing properties na ni udongo asili haujachanganya na kitu, unasaidia kuponya ngozi na kuirudisha katika hali yake ya kawaida. Wengine wanautumia kupaka kwenye nywele na hata katika mwili mzima. Chukua tu huo udongo changanya na maji upate paste nzito then paka usoni, ikikauka nawa then paka moisturizer.


Tumia Full Fat Yogurt.

Nimesoma sehemu kauwa kuna culture zingine wanawake wanatumia full fat milk/yogurt kupaka usoni ili kufanya ngozi zao ziwe nyeupe, na wanadai kuwa inafanya kazi. Hivyo tumia maziwa/mtindi ule fresh ambao haujatolewa mafuta wala kitu chochote, unapaka usoni angalau mara 2 kwa wiki kama face mask ya kawaida. 

Wengine hutumia greek yogurt nadhani zinapatikana supermarkets

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...