Thursday 24 August 2017

AD2 Fangasi ni nini Watu wengi hawajisikii vizuri unapokuja wakati wa kuzungumza juu ya fangasi kutokana na namna ugonjwa wenyewe unavyochukuliwa na jamii. Hii inatokea sababu mara nyingi ugonjwa huu hutokea sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani. Fangasi mara nyingi inawapata zaidi watu wanaoishi kwenye maeneno ya joto kuliko wale wanaoishi maeneno ya baridi kutokana na vimelea vya ugonjwa wenyewe kushamiri zaidi sehemu za joto. Pamoja na hayo yote fangasi ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, mimi mwenyewe nimewahi kupatwa na fangasi sehemu za siri na zilinisumbuwa sana. Takwimu zinadai katika kila watu watano mmoja kati yao anapatwa na maradhi haya katika safari yake ya kuishi kwa hapa Tanzania. Hapo awali fangasi walikuwa wanahesabika kama ni aina mojawapo ya mimea lakini baadaye sayansi imekuja kugunduwa kuwa fangasi hawana sifa za kuwekwa katika kundi la mimea. Kuna fangasi wa aina nyingi lakini tunaweza kuwaweka kwenye makundi makubwa mawili ambao ni fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi. Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi vimegawanyika tena katika sehemu kuu mbili, kundi la kwanza ni wale wanaojulikana kwa kitaalamu kama dermatophytes au dematofaiti kwa kiswahili na hamira au yeast kwa kiingereza Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu, basi leo fahamu kuwa hamira yaani hamira ile inayotumika wakati wa kupika maandazi na hata mikate ni fangasi. Fangasi huishi kwenye ngozi kwakuwa hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi ambayo huitwa keratini (keratin). Keratini ni protini ya muhimu sana katika ngozi na inatengeneza asilimia kubwa ya ngozi, kucha na nywele ambako kama umeshagundua mpaka sasa ni sehemu ambazo fangasi hupenda sana kushambulia kuliko sehemu nyingine za mwili. Kwahiyo utagundua kuwa sababu kubwa ya waTanzania wengi kuugua fangasi ni hii protini ya kwenye ngozi ijulikanayo kama keratini, joto na uwepo wa hali ya unyevu unyevu katika maeneno mengi hasa ukanda wa pwani. Kwa hali ya kawaida, fangasi wa aina hii huwa hawana madhara makubwa, wao huweka makazi yao tu kwenye ngozi bila kusababisha hali yoyote ya madhara kwenye ngozi. Madhara ya vimelea hivi huonekana baada ya idadi kubwa ya vimelea hivi kuongezeka kwenye eneo dogo moja la ngozi. Fangasi ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ikiwa watu hao watashirikiana mavazi na vifaa vingine vya usafi wa mwili. Madhara ya Fangasi katika ngozi Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele. Aina za maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi Kuna aina nyingi za maradhi ya ngozi ambayo chanzo chake huwa ni fangasi na hayo yote yameganwanywa katika sehemu kuu mbili: Share AD3


AD2
Fangasi ni nini
Watu wengi hawajisikii vizuri unapokuja wakati wa kuzungumza juu ya fangasi kutokana na namna ugonjwa wenyewe unavyochukuliwa na jamii. Hii inatokea sababu mara nyingi ugonjwa huu hutokea sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani.

Fangasi mara nyingi inawapata zaidi watu wanaoishi kwenye maeneno ya joto kuliko wale wanaoishi maeneno ya baridi kutokana na vimelea vya ugonjwa wenyewe kushamiri zaidi sehemu za joto.

Pamoja na hayo yote fangasi ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, mimi mwenyewe nimewahi kupatwa na fangasi sehemu za siri na zilinisumbuwa sana. Takwimu zinadai katika kila watu watano mmoja kati yao anapatwa na maradhi haya katika safari yake ya kuishi kwa hapa Tanzania.

Hapo awali fangasi walikuwa wanahesabika kama ni aina mojawapo ya mimea lakini baadaye sayansi imekuja kugunduwa kuwa fangasi hawana sifa za kuwekwa katika kundi la mimea.

Kuna fangasi wa aina nyingi lakini tunaweza kuwaweka kwenye makundi makubwa mawili ambao ni fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi.

Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi vimegawanyika tena katika sehemu kuu mbili, kundi la kwanza ni wale wanaojulikana kwa kitaalamu kama dermatophytes au dematofaiti kwa kiswahili na hamira au yeast kwa kiingereza

Kwahiyo kama ulikuwa hufahamu, basi leo fahamu kuwa hamira yaani hamira ile inayotumika wakati wa kupika maandazi na hata mikate ni fangasi.  Fangasi huishi kwenye ngozi kwakuwa hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi ambayo huitwa keratini (keratin).

Keratini ni protini ya muhimu sana katika ngozi na inatengeneza asilimia kubwa ya ngozi, kucha na nywele ambako kama umeshagundua mpaka sasa ni sehemu ambazo fangasi hupenda sana kushambulia kuliko sehemu nyingine za mwili.

Kwahiyo utagundua kuwa sababu kubwa ya waTanzania wengi kuugua fangasi ni hii protini ya kwenye ngozi ijulikanayo kama keratini, joto na uwepo wa hali ya unyevu unyevu katika maeneno mengi hasa ukanda wa pwani.

Kwa hali ya kawaida, fangasi wa aina hii huwa hawana madhara makubwa, wao huweka makazi yao tu kwenye ngozi bila kusababisha hali yoyote ya madhara kwenye ngozi. Madhara ya vimelea hivi huonekana baada ya idadi kubwa ya vimelea hivi kuongezeka kwenye eneo dogo moja la ngozi.

Fangasi ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine ikiwa watu hao watashirikiana mavazi na vifaa vingine vya usafi wa mwili.

Madhara ya Fangasi katika ngozi
Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele.

Aina za maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi

Kuna aina nyingi za maradhi ya ngozi ambayo chanzo chake huwa ni fangasi na hayo yote yameganwanywa katika sehemu kuu mbili:
AD3

1 comment:

  1. Tiba ya VVU / Ukimwi imekuwa inapatikana kwa muda mrefu kupitia. Iyabiye, hutenda na kutibu VVU. Ni tu kwamba watu hawakujua kuhusu hilo na kwamba hawajui cha kufanya na VVU. Unaweza kufikia daktari kupitia: iyabiyehealinghome@gmail.com au Whatsapp na simu: +2348072229413

    ==================================

    The Cure for HIV / aids has been available for a long time from Dr. Iyabiye, he treats and cures HIV. It's just that most people didn't know about it and even those people that was treated and cured didn't testify or notify people about it because they don't want to be known to have lived with HIV before. You can reach the doctor through: iyabiyehealinghome@gmail.com or WhatsApp and phone call: +2348072229413

    ReplyDelete

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...