Sunday 7 January 2018

je umewahi kusalitiwa na best friend wako? ulijifunza nini?



leo tuongelee ushosti jamani. mie ni muhanga wa kusalitiwa na best friend zangu sio mara moja wala sio mara mbili. nikajikuta siamini tena rafiki kabisa na mpaka sasa sina rafiki wa kusema tumeshibana. mashosti tunakutana tu kwenye vikundi tuna have fun basi. simpi mtu nafasi ya kunijua sana undani.
kabla sijaolewa nilikua na shost namuambia kila kitu changu. kumbe yy anamwambia boyfriend wangu kila kitu. nikashangaa jamaa kakata kamba ghafla na sikujua. nikapata mwingine nikajua huyu ndio tunaoana. nikawa namueleza shost mipango yangu yote! hee akamtafuta jamaa akawa anampa maneno weee mpaka jamaa nae akanitema. Mungu akanisaidia nikapata mwingine nikajifunza kuwa msiri, yule BF aliyepita alivyoona naolewa ndio akaja kuniambia shoga ako ndio alitugombanisha! baadae tena nikakutana na yule mwingine akanieleza hicho hicho! nilijuta!
hivi mwanamke ukimuharibia mwenzio unafaidi nini? hebu tujadili maana haya yanafanyika maofisini, kwenye biashara kila mahali, shida nini? pole kwa gazeti

MAONI YA MDAU
yani mm nina hadi CV ya kusalitiwa saaana na friends..lakini Mungu anavyowachapa vibao nawatizama tu..wanakonda na kupauka kwa stress namna ya kuomba msamaha wanashindwa….wanabaki kukuongelea pembeni weeee….me nina friend ye hatak hata siku moja awe chini yako..yan mjuaji yeye…kila kitu yeye uwe na kitu kizuri atapooonda baada ya week unamuona nacho..uwe na mwanaume atapoooonda mara mnene…mara kitambi…mara mbona gari yake hivi…cha ajabu sasa yeye anapata vimeo kila siku vina mla hapati hata hata interest basi…akirudi anabaki tu yule jamaa angu anapesaaa sijui nn…sasa unabaki kujiuliza anapesa si angekutoa huku uliko?mie nipate sasa wa maaana ananuuuna kwanza atanza linganisha na wa kwake ahahhha sa hivi kabaki kuweka status za kizungu madooongo high quality…kwan nahangaika basi?kabaki analaani tu..mm yananinyookea…na kumtegemea Mungu/Allah kuna faida haswaaaaaa..waaibishwe wote wanaoninenea mabaya pasipo na ulazima

Sioni umuhimu wa kuwa na rafiki au marafiki nawaonaga ni vimeo kwangu, ila tuacheni utani sisi wanawake tuna roho mbaya yani unaweza kumuamini rafiki kumbe ni bonge la mnafiki. kuna mdada mmoja huku job anapendaga umbea hatari sijui hili wala lile kumbe kuna mambo yangu huwa namwambiaga kumbe maneno anayasambaza baada ya kumjua ni mmbeya nikafunga mdomo wangu nikatokeaga kumchukia akijaga ofisini anaanza kuniambia eeh nipe umbeya toka siku hio nikalitemea mbali

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...