Tuesday 17 October 2017

MLO WA ASUBUHI KWA ANAYEPUNGUZA UZITO

Wiki moja iliyopita nilisema ntakuwa nashare namna mbalimbali ya kuandaa ratiba ya mlo wa asubuhi,mchana na usiku.Tulianza na mlo wa asubuhi na nikapata maoni ya wale wanaotaka kupunguza uzito je wanaweza kuwa na ratiba ipi?Ifuatayo ni ratiba ya mlo wa asubuhi kwa mtu anaetaka kupunguza mwili/uzito.
JUMATATU
Mkate wa brauni
slesi 1 +siagi ya karanga
Yai 1 la kuchemsha
Kinywaji cha soya
Chungwa 1
JUMANNE 
Mhogo/kiazi/gimbi
kipande 1
Kachumbari-nyanya na
kitunguu na tango
Maziwa kikombe 1
Papai
 JUMATANO 
 Sandwich (mkate
brauni slesi 2,yai la kukaanga moja,nyanya kitunguu,hoho,tango)
Chai ya maziwa yenye
viungo

Tikiti maji
ALHAMISI
Chapati 1 ya unga wa
atta (roti-iliyochomwa bila mafuta)
Sausage 1
Kinywaji cha Soya
Parachichi

IJUMAA
Uji wa dona na maziwa/oats
na maziwa/all bran na maziwa(kula kimojawapo)
Tikitimaji
JUMAMOSI 
Supu ya
kuku/samaki/nyama
Chapati 1 ya unga wa
atta (roti-iliyochomwa bila mafuta)
Saladi ya matunda
JUMAPILI 
Skonzi za atta
+cheese/asali/siagi ya karanga
Salad ya mboga
mboga(nyanya,tango,kitunguu)
Maziwa kikombe 1
Nanasi
NOTE
·       
Maziwa yatakayotumika yawe yaliyoenguliwa mafuta
yaani skimmed milk,unaweza chemsha na kuondoa mafuta yatakayobaki juu au
ukatumia maziwa ya Cowbell.
·       
Matunda na mboga mboga zitumike za kwenye msimu,
mboga na matunda yanayoshauriwa zaidi kwa kupunguza uzito ni spinach, sukuma
wiki, lettuce,tango,nyanya,zabibu,chungwa,limao,parachichi,papai,apple,tikitimaji,cauliflower,broccoli,bilinganya,nyanyachungu,bamia,uyoga,zukini
na maharage mabichi.
·       
Tumia unga wa nafaka zisizokobolewa, dona-inga
wa mahindi mazima, atta-unga wa ngazo isiyokobolewa
·       
Roti jina
la aina ya chapatti ya Kihindi inayochomwa kwenye kikaango bila mafuta.
·       
Usile mayai kila siku, yana lehemu, mayai matatu
kwa wiki yanatosha
Kuna namna mbali mbali za kuandaa mlo wako wa asubuhi iwapo unafanya diet ili kupunguza uzito.Wataalamu wanasema sio vizuri kutokula kabisaa hasa mlo wa asubuhi kisa unataka kukonda.Kula ni muhimu ila unakula nini?Hii aametuandalia mdau Valeria Millinga.Ikipatikana ingine ntaweka pia

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...