Friday 13 October 2017

Leo ningependa kuzungumzia urembo kwa WANAWAKE.....!


Urembo kwa wanawake ni jambo lisiloepukika na inahitaji gharama kwa mwanamke kujiweka katika hali ya utanashati ili kuwa presentable na kuleta mvuto wa kimapenzi kwa wanaume.

Hapa chini nitajaribu kuelezea mambo ambayo mwanamke anatakiwa kuyazingatia anapojiremba.


Mwanamke kutinda nyusi..... Kwa wale wenyeji wa Tanga wanayajua mambo hayo vizurti sana. Madame B anahusika naamini anaweza kuanzisha darasa hapa na wanawake mkanufaika.

[​IMG]

Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona Smile kapendezshwa na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha..........


[​IMG]


[​IMG]

Rangi ya mdomo nayo ni eneo lingine linalompendezesha mwanamke. Ukweli ni kwamba tunatofautiana sana midomo wazungu wanaita Lips. Kila mwanamke ana tofautiana Lips na mwingine kwa hiyo hata rangi ya midomo nayo inakwenda sambambana aina ya lips na rangi ya ngozi ya mwili aliyo nayo mwanamke, siyo unajisiriba rangi ya mdomo halafu unaonekana kituko. Wasiliana na wataalamu wa urembo kwa ushauri zaidi.


[​IMG]

Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu. Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha kwa kung'atwa au kwa kuliwa na fangasi. Ipo aina fulani ya fangasi ya kwenye kucha inawashamblia san wanawake hususan kwa hapa Dar, sijui ni kutokana na maji kwa sababu ya kufua au kuosha vyombo au kitu kingine. Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona tabibu mtaalamu wa ngozi kwa msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa. Au akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue kusitiri aibu.


[​IMG]

Marashi, manukato au unyunyu kama wanavyoita vijana wa mjini ni muhimu kwa wanawake lakini ni vyema nikaweka angalizo. Haipendezi kwea mwanamke anayepulizia manukato yanayonukia sana mpaka yakawakera wengine. Unaweza kupishana na mwanamke ukadhani umepishana na jini subiani kwa jinsi anavyonukia. Kwa wale wenyeji wa Tanga wanajua vizuri kuhusu uhusiano uliopo kati ya makukato na majini. Ni vyema wanawake wakajipulizia marashi yenye staha na yasiyokera.


[​IMG]

Nywele za kwapa na kule kunako Va jay Jay ni vyema zikanyolewa. Kuna baadhi wanawake unaweza kukutana nao kwenye daladala wamevaa blouse kata mikono wakinyanyuo mikono kushika juu ya bomba kama wamekosa siti utatamani kuteremka kwenye daladala maana wamejaa nywele za kwapa halafu hicho kiharufu kinachotoka hapo... mh!!! Majanga kwa kweli.




[​IMG]

Ngozi ya mwanamke ni sensitive sana na inaakiwa ipakwe aina ya mafuta au lotion yenye virutubisho kulingana na aina ya Ngozi. Kuna wanawake wenye Ngozi ya mafuta (Oil Skin) kuna wenye Ngozi mchanganyiko (Combination Skin) na kuna wale wenye ngozi kavu (Dry Skin). Ni vyema mwanamke kujua aina ya ngozi yake ili ajie aina ya product ya ngozi anayopaswa kutumia na siyo kwa sababu umemuona Paloma anapaka aina fulani ya lotion na wewe unakimbilia kununua. Omba ushauri kwa wataalamu wa ngozi watakusaidia. Kuna baadhi ya maduka yanyouza vipodozi wanatoa msaada huo bure au unaweza kuwasiliana na Lady doctor, Lisa au Nivea

[​IMG]

[​IMG]

Urembo wa Nywele ni muhimu sana. kuna baadhi wanawake hawajui ni mtindo gani wa nywele unawapendeza. eti kwa sababu kamuona lara 1 kanyoa nywele na kuacha kipara na yeye anataka kufanya hivyo wakati ana kichogo kirefu. utachekesha walionuna. Inatakiwa kabla ya kutengeneza nywele uzingatie rangi ya ngozi ya mwili wako na kichwa chako kikoje. Unaweza kukuta mwanamke ni mweusi kama Madame B halapu amevaa wigi la rangi ya Gold. Majanga......!!!!!! Kuna wataalamu wa kutengeneza nywele wanaoweza kukushauri namna ya kutengeneza nywele zako ukapendeza. Waone kwa ushauri au wasiliana na snowhite kwa msaada zaidi

[​IMG]


[​IMG]

Vivazi navyo ni muhimu kwa wanawake kulingana na aina ya mtoko, siyo mwanamke anavaa wakati wa mtoko kama vile anakwenda kununua Ice Cream kwa Mpemba. Ni vyema mavazi yakapanmgiliwa kulingana na umbo la mwanamke. Kuna baadhi ya wanawake wanapenda kuvaa mavazi yanayowabana wakati maumbo yao ni kituko. Kwa nini usitafute ushauri kwa wataalamu wa mavazi wakakushauri.


[​IMG]

mazoezi ni muhimu kwa mwanadamu kwa ajili ya kuuweka mwili katika hali nzuri kiafya, lakini wengi wetu tumekuwa wavivu sana kufanya mazoezi hata ya kutembea. Kwa upande wa wanawake wa hapa nchini hili ni tatizo kubwa. Wanawake wengi hapa nchini ni wavivu katika kufanya mazoezi na ndio sababu wengi wana vitambi na hivyo watu wengi kudhani kwamba wana ujauzito.

Urembo kwa mwanamke unajumuishwa na muonekanao wa mwili kama umekaa katika shepu nzuri. Sura siyo hoja sana, bali maumbile. kuna baadhi ya wanawake wamejaaliwa kuwa na sura na maumbo mazuri lakini baada ya kufakamia bia na nyama choma hususan kiti moto huumuka na kuwa na maumbo makubwa na mabaya yasiyo na mvuto.

Mazoezi hayahitaji gharama, maana wengi hapa watakuja kulalamika kwamba hawana fedha za kwenda Gym. Kwa wale walioko Dar na wanaofanya kazi maeneo ya mjini nawaalika waje wajiunge na Club yetu ya mazoezi ya kutembea jioni kuanzia Jengo la Exim Tower kuzunguka Gymkhana Club kupitia ufukwe wa bahari ya Hindi hadi Palm Beach kisha tuna pita barabara ya Umoja wa Mataifa mpaka Diamond Jubilee kisha tunatokea mahakama ya Kisutu na tunamalizia pale Exim Tower kila siku za kazi kasoro siku za Jumamosi na Jumapili. Hakuna Kiingilio na parking ipo. kwa anayetaka anaweza kuwasiliana na mimi kwa PM........

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...