Saturday, 16 September 2017

MUONGOZO WA KITAALAM WA JINSI YA KUWA NA NGOZI NZURI

Ili kuwa na ngozi nzuri au kuondoa matatizo mbalimbali ya ngozi unatakiwa kujua mambo ya kufanya na vipodozi vya kutumia ili kufanikisha malengo yako. Mambo mbalimbali kama vile kutumia vipodozi vizuri na vinavyoendana na ngozi yako, kula chakula bora, kunywa maji ya kutosha, kusafisha uso vizuri, kutumia vipodozi na dawa nzuri kwa ajili ya kulainisha ngozi na kuondoa matatizo mbalimbali ya ngozi, kuepuka jua kali, kupumzisha ngozi na kadhalika husaidia kuifanya ngozi kuwa nzuri na kuondokana na matatizo mbalimbali kama vile chunusi, michirizi, makunyanzi, mafuta mengi usoni, ngozi kavu, madoadoa, makovu nk
JINSI YA KUWA NA NGOZI NZURI
Ili kuwa na ngozi nzuri cha kwanza kabisa jua mambo yanayoharibu ngozi na yale yanayopendezesha ngozi yako kisha fanya mambo yanayopendezesha ngozi na epuka yale yanayoharibu ngozi yako
Mambo yanayopendezesha ngozi
1. Chakula bora na matunda
2. Mazoezi
3. Usafi wa kutosha
4. Vipodozi vizuri, vinavyoendana na ngozi yako
5. Kunywa maji ya kutosha
Mambo yanayoharibu ngozi
1. Jua kali
2. Vipodozi vikali na visivyoendana na ngozi yako
3. Kukosa usingizi wa kutosha
4. Msongo (Stress)
5. Maambukizi ya vijidudu na magonjwa ya ngozi
6. Majeraha
7. Uchafu unaobaki kwenye ngozi
HAKUNA SIRI NYINGINE ZAIDI YA HAPO
Hakuna siri. Hakuna kabisa! Kilichobaki ni kujua kwa usahihi kabisa mambo yafuatayo:
1. Aina ya ngozi yako
2. Vipodozi vizuri kwako na vile vinavyoendana na aina ya ngozi yako
3. Jinsi ya kutumia vipodozi hivyo kwa usahihi ili kupata matokeo mazuri na ndani ya muda mfupi
4. Chakula bora ni kipi na matunda gani ni mazuri zaidi kwa ngozi yako
5. Vipodozi na dawa nzuri kutumia kwa ajili ya kuondoa chunusi, madoadoa, mafuta mengi usoni, makovu, harufu mbaya, michirizi, makunyanzi, kutibu ngozi kavu na kadhalika
6. Maji ya kutosha kwako ni kiasi gani
UMEKWAMA? TUPO TAYARI KUKUSAIDIA
Kila mtu ana ngozi yake na mahitaji yake, ndio maana watu tofauti hupata matokeo tofauti hata wakitumia njia au vipodozi vinavyofanana. Hivyo, tunashauri watu mambo mbalimbali na vipodozi mbalimbali kulingana na aina za ngozi zao, matatizo yao na mahitaji yao.
PATA USHAURI NA TUMIA VIPODOZI KULINGANA NA AINA YA NGOZI YAKO, TATIZO LAKO NA MAHITAJI YA NGOZI YAKO
Hii ndo siri kubwa zaidi ya kupata matokeo mazuri zaidi, kwa haraka zaidi na kwa gharama nafuu sana. Pia inakusaidia kuepuka madhara.
PATA MAFUNZO YA ANA KWA ANA NA KWA KWA VITENDO
Kama upo Dar es salaam basi una bahati sana na hauna haja ya kuhangaika tena unapohitaji vipodozi vizuri, kutunza na kuipendezesha ngozi yako vizuri na kuondoa matatizo mbalimbali katika ngozi yako maana tunafundisha ana kwa ana. Kila jumamosi kuanzia saa 4 kamili asubuhi tunatoa mafunzo hayo yote kwa kikundi cha watu. Karibu sana uungane na wenzako na tutakusaidia kwa ukaribu zaidi.
Utachangia Tsh 3,000/= tu kwa ajili ya ukumbi na maendeleo ya programu hii.
Weka nafasi yako mapema. Jiandikishe sasa.
Tuma meseji yenye neno“MAFUNZO” kwenda namba 0784082847 kisha utapigiwa na kuandikishwa.
Tunakupenda zaidi. Tunakujali zaidi.

No comments:

Post a Comment

Toa Weusi Kwa (Pubic Areas) Mapajani na Kwapani Kwa Kutumia Hizi Simple Ingridients

Kuwa na Mapaja meusi au kwapa jeusi kweli ni issue wanayoface wanawake wengi sana so usishangae wala kwasababu ur not alone,mtu unakuwa na ...